Msaada kwa mdau rafiki yetu
Nimejikuta njia panda baada ya meneja wa kampuni yetu (Mwanamke) kuniwekea mazingira magumu kwenye swala langu la kuoa. Hivi karibuni niliitisha michango ofisini kwetu kwa ajili ya ndoa ambayo nakaribia kuifunga soon, wafanyakazi wote walifurahi na kuahidi kutoa michango ya kutosha kasoro boss wangu ambaye amekuwa kinyume sana na swala langu la kuuoa
Sijawahi kutembea nae, wala kuwa na mahusiano mengine nje ya kazi lakini amekuwa na wivu sana mpaka inafikia wakati hanipi ruhusa kwenda kwenye mafundisho ya ndoa na hata jumamosi ananipangia majukumu nikose muda.
Mwezi uliopita tulipangiwa tuende kwenye uzinduzi wa tawi letu jipya la kampuni basi akaniweka kama mtu muhimu kuhudhuria uzinduzi huo pale Singida kila mtu alishangaa maana sikutakiwa kuhudhuria kutokana na position yangu.
Nashindwa kulalamika kwa mkurugenzi sababu meneja huwa anifavour sana zinapotokea posho ofisini ( hii ni kabla ya kufanya maamuzi ya kuoa), mafuta ya kavits kangu town amenisaidia sana, mikopo n.k
Nimekosa raha sana ni kama ananikomoa , ni mke wa mtu na anawatoto na pia amenizidi umri. Wengi wamenishauri nimuulize ni kwanini anafanya hivyo lakini nahisi ntachochea moto
Naombeni msaada wa kimawazo kwani swala hili linanitesa ndugu zangu
Halafu umeuliza maswali rahisi sana ambayo hata ukijijibu mwenyewe kimoyo moyo, majibu yake yangelikuwa ni hayo hayo 100%!
Duniani kote unapotaka kufanya jambo lolote la maana halafu jambo hilo likaingia viral, kulifanikisha lazima utumie nguvu nyingi, vinginevyo linavurugwa na kufa, tena na watu ambao hauwezi kutarajia!
Halafu huyo boss unaona anakupiga vita!
Wewe unaona hiyo ni vita kweli?
Nikwambie hiyo siyo vita wala siyo chuki, hayo ni mambo ya kibinadamu tu.
Haujasikia usemi usemao "hakuna binadamu aliyekamilika"?
Hayo nina uzoefu nayo na nitakupa mfano:
Tulipopata ajira, ofisini tulimkuta mama mmoja siyo boss, ni staff mwenzetu tu, kwanza alinitia jakamoyo kwa kutomuelewa.
Alinionesha haiba mbili kwa pamoja, yaani kunichukia sana na kunipenda sana kwa wakati mmoja!
Yaani tukiwa wawili ananichangamkia sana, lakini tukiwa wengi hajibu hata salamu zangu na nikawa nasikia kwa watu anawatangazia anavyonichukia!
Sasa enzi hizo nilikuwa mhuni halafu mjanja nikaona jambo hilo nilifanyie utafiti kuupata ukweli, nini tatizo, tabu iko wapi kwa mtu ambaye hanijui, simjui?
Alternative ya kwanza nikaona nimtongoze huyu mama mtu mzima na akinikataa nijue kweli ananichukia, hivyo nimburuze kwenye uongozi na visa vyake nisivyovielewa, ili akaeleze nilichomkwaza!
Nikamvizia sehemu nikampandia sound, alivyosikia matamshi yale kutoka kinywani mwangu, haiba yake ikabadilika ghafla hadi nikashangaa!
Tabasamu pana, furaha tele moyoni na cheko la wazi!
Kilichofuata sikielezi hapa, isipokuwa nachotaka kukueleza ni kuwa si kila mtu unayehisi kuwa anakuchukia, yaweza kuwa ni kinyume na unavyomfikiria!
Anaweza kuwa "hakuchukii kwa ubaya".
Na kwamba, jambo la heri unalotarajia kulifanya hivi karibuni huwa linaibua hisia za watu, wengine kwa husda na wengine kwa wivu tu kuwa "wa kuoa awe huyu", basi kijicho!