Boss wa Diamond akubali kushiriki kwenye ushirikina

Boss wa Diamond akubali kushiriki kwenye ushirikina

Nanukuu..

""sijawahi kuwa na sina bifu na alikiba""

""kila mtu anahaki ya kumchagua amtakae, uzalendo haununuliwi bali unatoka moyoni kwa mtu husika, kama unampigia davido au yeyote yule ni haki yako lakini kama unaona tuzo inafaa ije bongo nipigie""

""Nadhani mabishano ya mashabiki juu yetu sisi kwa sisi hayawezi kutupeleka popote, imefika wakati wafananishe wanamuziki wetu na davido, wizkid etc. ""

""unapoamini masuala ya ushirikina unamkosea mwenyezi Mungu, sina imani juu ya mambo hayo, ña mimi anachoamini babu tale siwezi sema nimzuie, kila mtu anahaki ya kuamini anachokiamini""

""Nguvu za wanaonichukia na kupiga kura kwa davido, ni bora pia wangetumia nguvu hiyo kuwapa support zaidi wasanii wetu,, mwakani tuwe na wawakilishi zaidi ya wawili""

""Huwa simtozi mtu pesa yeyote kwenye collable, na wala sijawahi tozwa... Nimefanya collable karibu na A list wote wa Afrika, nyimbo nyingi zipo tayari baadhi tu zinasubiri wakati wake kufanya video shoot, hata hivyo haziwezi kuachiwa achiwa tu, sababu tunataka kila mwaka mziki wetu uwepo kwenye chati kubwa za muziki""

baadhi ya alivyoongea president wa wasaaaaaaaaafi.... Mr. Icon

Aaache ushirikina mxiuu mtoto mdogo mchawi roho,yani watu ambao hawajaenda shule wanapenda sana ushirikina na ipo siku mungu atawaumbua mbwa hawa
 
So because Tale was open about his beliefs watu naona moja kwa moja mnamlink na Diamond. Hapa ndio huwa ufinyu wetu wa akili unapodhihirika. How many of you here actually believe in Witchcraft? Nani hapa anaamini unaeza ukalogwa kabisa mambo yako yakashindikana au ukalogwa ufe na ukafa kikweli? Diamond ni mshirikina, oh yeah alipokua anauza mitumba all those years hizo ndumba zilikua hazifanyi kazi? If his success is down to witchcraft, vijana walivyo na tamaa Tanzania leo hii washindwe nini kumiminika kwa witch doctors? Kuwenu mnafikiria before accusing people.

Actually it looks like what Tale actually meant is he believes in traditional medicine and healing. I don't think he meant eti yeye anaamini witchcraft and that he goes to waganga kuchawia.

Aisee mtoto wa watu kaandika nyimbo zake, katoa miziki yake imependwa na watu and he then used the opportunity to make himself a brand. Mtamsingizia kalala na mama yake, sijui kalala na paka but hey it doesn't make it true.

chukua gwara
 
Diamond apo awali aliwahi kuhusishwa na ushirikina, walisema sijui kalala na mama ake ,sasa tetesi za namna hii na kauli ya tale leo inaleta picha mbaya, kama Mungu akiamua kukubaliki utabarikiwa tu, ila kama umeamua kufanya ushirikina mwisho wake upo yetu macho

Binamu kuamini uchawi kwa tale huwezi kumjumlisha n chibu uchawi ustoshe tale kaongea kma tale.....sisi ngozi nyeusi m2 akitoka kimaisha maneno lazma yasemwe 2 sikatai wa2 wanaloga sana ila haiwasaidii mana mafanikio yanakua mda mfupi.
Zamani mererani wa2 walikua wanaloga c mchezo yani laana tupu.

Hao walogaji wote walipata pesa ila sasa wamekita hawana hata mia wengine wameuza kila ki2.mgodi ukiwekeza hela na ukawa na geologist mzuri lazma upate madini iwe isiwe na ndio wengi kwasasa wanafanya hivyo....ushirikina haukufikishi popote
 
mambo ya ushirikina , mtu akipata mshahara anakula bata zikiisha utasikia kuna chuma ulete hapa
 
Diamond yupo vizuri kwenye interview za one to one. .anayemchemshaga mara nyingi ni salaam
 
Hata mimi nimemsikia akisema hivyo.

Walau yeye kawa muwazi ingawa naona anajihangaisha tu na hayo mambo yasiyo na uthibitisho wowote ule.
 
MMh ebu usitufanye watoto apa, kwa hyo na wewe unajifanya hujaelewa?? Diamond mshirikina toka zamani, we waache tu ipo siku yatamkuta, ata ajulikane dunia nzima ila mwisho wake sio mzuri, mtoto mdogo anakuwa mchawi, yani babu tale katufungua macho
ha ha ha ha
Kamu ulize wema kama diamond ni mchawi ama laa!
 
Hakuna cha ajabu wengi waafrika bado hawaendi hospitali wanakimbilia waganga wa jadi kutibiwa na ndio maisha wanakua nayo.

Kwenda kwa mganga kwa wengi haimaanishi wameenda kugangia watu au maisha yao.
 
Diamond apo awali aliwahi kuhusishwa na ushirikina, walisema sijui kalala na mama ake ,sasa tetesi za namna hii na kauli ya tale leo inaleta picha mbaya, kama Mungu akiamua kukubaliki utabarikiwa tu, ila kama umeamua kufanya ushirikina mwisho wake upo yetu macho

Hyo ya kulala na ........ Ilienea sana tu yani sijui kusafisha nini, huyu babu tale zaidi ya kufitinisha mambo yake na wasanii ni mzee wa kukurupuka. Kuna kauli hazipaswi kuzungumzwa hadharani hata ka unazifanya.
Maana kwa ushirikina babu tale ni hatari. Next time afikirie kabla ya kuongea inaharibu sifa. Si ajabu kwa uelewa wake anajua ushirikina ni ujanja kikija kubuma ndo kuumbika maxima. Ushirikina ni hatari.
 
i concur with you Diva Beyonce katika hili Tale kateleza kabisa maana hii itamlenga Diamond sana kuliko yeye binafsi!

Kwakweli alitakiwa kujua yeye ana position gani kwa jamii na image yake ina muwakilisha nani? Ni ngumu watu kutenganisha ushirikina wa kufanikisha mambo yake binafsi na mambo ya Diamond hasa muziki!

Kwakweli hii kauli itamuathiri sana Diamond maana aliyesema ana yaamini haya ni manager wake mimi naamini shughuli za music wa Diamond zinafanikisha shuguli binafsi za Babu Tale!

Hii si mala yake ya kwanza kuropoka huu anao huita ukweli wake..kwakweli una muathiri Diamond zaidi kuliko yeye binafsi kama anavyo sema!

Mimi nafikiri Babu Tale anatakiwa kufunzwa nini cha kuongea kwenye media na ambacho si cha kuongea....!

Kuna watu kama T.I.D na Q -chillah walisha toa tuhuma zilizo kuwa zinaelekea kwa Diamond kuwa ana waroga..Mimi sijawai kuamini haya lakini huu ujinga wa Babu Tale unawapa sababu na credit kuamini kuwa kuna ushirikina kwenye maendeleo yake jambo ambalo lingeweza kuzuilika!

Binafsi naona huu ni ujinga wa Babu Tale ambao una muharibia Diamond reputation yake......
 
Last edited by a moderator:
Diamond apo awali aliwahi kuhusishwa na ushirikina, walisema sijui kalala na mama ake ,sasa tetesi za namna hii na kauli ya tale leo inaleta picha mbaya, kama Mungu akiamua kukubaliki utabarikiwa tu, ila kama umeamua kufanya ushirikina mwisho wake upo yetu macho

MMh ebu usitufanye watoto apa, kwa hyo na wewe unajifanya hujaelewa?? Diamond mshirikina toka zamani, we waache tu ipo siku yatamkuta, ata ajulikane dunia nzima ila mwisho wake sio mzuri, mtoto mdogo anakuwa mchawi, yani babu tale katufungua macho

Kwa mtazamo wenu inaonekana mnaamini mafanikio ya Diamond ni kwa sababu ya ushirikina, kama ni hivyo basi ushirikina una nguvu sana kiasi kwamba kaweza kuroga Afrika nzima kiasi cha kumfanya kuwa msanii wa kimataifa, anayekubalika ndani ya Afrika na nje ya Afrika.
 
Pengine wana haki ya kuamini hivyo maana haingii akilini manager ambaye ana msimamia msanii ana kiri kuwa ana amini ushirikina halafu watu wakawaida wasi doubt kama ana kwenda kwa waganga kufanikisha kazi za msanii wake au lah!

Mimi ninacho jaribu kusema kuwa hii kauli ya Babu Tale ina mchafua Diamond maana Diamond anaweza akawa haamini kabisa na hataki kushiriki lakini watu anao watuma kumfanyia kazi zake wakitamka maneno kama haya ina leta picha mbaya sana na sidhani kama Diamond kafurahishwa na kauli hizi za Tale!

Tale ni mjinga anashindwa kutambua nafasi yake kwenye jamii!
 
Diamond Platnumz
alikuwa live kwenye XXL @CloudsFM, kuna vingi kaviongea Exclusive, nilipata nafasi kumsikiliza na hivi ni baadhi ya vitu alivyoviongelea leo June 6 2015. Unadhani Diamond anaamini uchawi >>> “Japokuwa vitabu vya dini vinasema ‘ndele’ zipo lakini haupaswi kuamini… Kuamini ni sawa na kumkiuka Mwenyezi MUNGU”>>> Kuna beef kati yake na Ali Kiba? Na vipi zile Team kwenye Mitandao ya Kijamii >>> “Sijawahi kuwa na beef nae hata siku moja… Sioni kama kuna ubaya wowote, kila mtu ana maamuzi kumchagua mtu anayemtaka yeye kumshabikia, huwezi kumlazimisha mtu” >>>

Wawachukue msanii fulani na msanii fulani wawashindanishe na wasanii wa nje, ukiwashindanisha wasanii wa Tanzania haiwezi kusaidia Industry yetu. Kuna malipo ya collabo >>> “Sijawahi kufanya malipo kufanya nyimbo na mtu yoyote.. Mwanzoni ilikuwa tabu, sasahivi wanafahamu kwamba kufanya nyimbo na Diamond inakuwa rahisi nyimbo kufahamika East Africa… nimefanya collabo na karibuni wasanii wote wakubwa Africa.” >>> Show ya MTV Road to MAMA Nigeria aliipataje? >>> “Ni mwaliko wa MTV, wa kwanza nilipewa South Africa nikafanya vizuri, wakaona wanipe na sehemu nyingine”>>> Diamond.

Hiki ndio alichojibu kuhusu kupigiwa kura za MTV Awards 2015 >>> “Wanaoona kuna umuhimu hizi Tuzo zije Tanzania waendelee kupiga kura, anayeona ni sawa kumpigia mwingine ni sawa… Uzalendo haununuliwi, huwezi kumlazimisha mtu” “Muziki wetu umekuwa na nafasi nzuri sana Africa, ni kazi kubwa sana imefanywa… Kuna utaratibu unaandaliwa kuona kama tutaweza kuwabeba watu kama mashabiki na Watangazaji.. Tupige kura kwa siku hata mara moja sio mbaya, kama tulichukua ‘Channel O’ sasa hivi tutashindwaje”

SOURCE: MillardAyo
 
Attachments

Mti wenye matunda haman jinsi zaidi ya kuvumilia Big up Mondi
 
ameulizwa ana amini uchawi kama upo kasema ndio

kaulizwa anashiriki kasema anashiriki yeye ni mwafrika na mtu wa morogoro so huwa ana enda kwa mganga kwa ajili ya mambo yke binafsi kama kupata tiba!

Hii haihusiani na diamond....!!

Yap kaka we umemuelewa vizuri hata mie nimemuelewa hivyo,mambo ya diamond hayana uhusiano kabisa na alichosema Babu Tale
 
Pengine wana haki ya kuamini hivyo maana haingii akilini manager ambaye ana msimamia msanii ana kiri kuwa ana amini ushirikina halafu watu wakawaida wasi doubt kama ana kwenda kwa waganga kufanikisha kazi za msanii wake au lah!

Mimi ninacho jaribu kusema kuwa hii kauli ya Babu Tale ina mchafua Diamond maana Diamond anaweza akawa haamini kabisa na hataki kushiriki lakini watu anao watuma kumfanyia kazi zake wakitamka maneno kama haya ina leta picha mbaya sana na sidhani kama Diamond kafurahishwa na kauli hizi za Tale!

Tale ni mjinga anashindwa kutambua nafasi yake kwenye jamii!

Mkuu nakubaliana na wewe na hata pia najisikia aibu sana Babu Tale kutamka kauli kama hiyo, ila katika akili ya kawaida, uchawi hauwezi kumfanya masanii akakubalika afrika nzima na sehemu za mabara mengine. Mafanikio ya Diamond hayawezi kuwa kwa sababu ya uchawi. Kwanza mimi binafsi sirogeki, hivyo hakuna namna ambayo Diamond kaniroga ili niupende mziki wake, na ninaamini hata kwa mashabiki wengine wa Diamond ni hivyo hivyo, hakuna aliyerogwa. Kwa staili hiyo, ushirikina hauna nafasi hapo.

Pia sote tunaona kwa macho yetu namna huyu kijana anavyohangaika kila kona ya dunia hii katika kupenyeza kazi zake, sasa kama suala ni ushirikina kwa nini asumbuke kiasi hicho wakati angeweza kutumia huo ushirikina ukampa umaarufu?
 
All in all Babu Tale kachemka uchawi sio sifa najua hata miongoni mwa tunacomment humu tumewahi kwenda kwa waganga lakini kwa zama hizi zilizo na mahospitali kila kona c sahihi kuendelea kuamini waganga wa kienyeji.
Inawezekana hao kina talle hawajajua ukubwa wa jina DiamondPlatinumz katika bara hili
 
babu tale kaongea ukweli ambao watu wengi mnauficha ila sirini mnajihusisha,hivi ni nani akivua shati ana chale either ulichanjwa utotoni ukiwa ujijui au umejipeleka mwenyewe kuchanjwa baada ya kuhisi usiku unapigishwa mzigo.hii inaonesha ishu za kishirikina zimetamalaki katika maisha yetu tusidanganyane
 
Kuna vitu havipaswi kuongea public babu tale leo nimemuona ----. AngeAcha tu anyway Diamond yy kajibu vzr.
 
Back
Top Bottom