Boss wa mke wangu ana moyo wa utu sana

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,472
Reaction score
9,542
Leo niliitikia wito wakwenda ofisini kwa mke wangu kuonana na boss wake kwaajili ya mazungumzo! Nimefika tumezungumza mambo mengi sana

Kubwa zaidi boss wake kasema nimruhusu mke wangu ampangie nyumba karibu na kazini ili awe anapata muda wakupumzika mapema nakufanya kazi zaidi maana ilikuwa inamlazimu aamke saa kumi usiku kuwahi kazini

Kwahiyo nyumbani atakuwa haji Kila jioni Tena kama ilivyokuwa awali! Atakuwa anakuja mara moja kwa wiki jumapili kwaajili ya kuniona na ibada. Nimekubali ombi la boss wake, jamaa alivyomkalimu kanipa na laki moja.

Mungu akubaribiki boss wa mke wangu
 
Au sio, nipe namba ya mke wako na mm nimchangie kidogo hela Kodi.
 
Tayari, ruksa ya kutandaza miguu imekubaliwa na fedha juu, laki moja imetolewa... ngoja wamchakate hadi achonge mzinga kwa ruhusa yako... Jiandae kwa maumivu...
 
Sitaweza kuzungumza mengi ila inajulikana wazi ukishaoa au kuolewa wote mnakua mwili mmoja.

Hivyo basi ili kupunguza ukali kidogo naweza kukwambia bosi wako anawaweka karibu yake ili muwe mnampa chakula kwa wakati... Huduma anayotoa mkeo kwa bosi wake ni inakua mmeitoa pamoja
 
Jambo la heri, ila usije kulalamika.

Mwalimu Nyerere alipata kusema kuwa, ukishaweka silaha chini usishangae kuwa mateka.
 
Jamaa ana upendo sana. Mheshimu sana.
 
We jamaa huo usingizi umelala embu amka haraka maana tunakoenda tunakuzika mchana kweupe. Shtuka.
 
Hii ni comedy original
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…