NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 11,297
- 14,588
Msimu wa 2025/26 unakaribia kwa kuanza, lakini jambo la kushangaza ni ukimya wa mfadhili mkubwa wa Simba SC, Mohammed Dewji (Mo Dewji). Mashabiki wengi wa Simba wanajiuliza, ni kipi kipya Mo Dewji anakiandaa? Au bado anatafakari mbinu mpya ya kuwashawishi na kuwadanganya kuhusu mafanikio ya msimu ujao?
Msimu uliopita ulijaa ahadi kubwa kutoka kwa uongozi wa Simba, ikiwemo bajeti ya mabilioni ya shilingi na usajili wa wachezaji wa kiwango cha juu, lakini matokeo yalikuwa tofauti kabisa na matarajio ya mashabiki. Hadi sasa, hakuna kauli wala mwelekeo rasmi kutoka kwa Mo Dewji kuhusu maboresho ya timu wala mkakati wa msimu mpya.
Mashabiki wa Simba wanahitaji ukweli, siyo porojo na matumaini hewa kama ilivyokuwa misimu iliyopita. Ukimya wa Mo unaweza kuwa ni sehemu ya mkakati wa kutengeneza simulizi mpya ya kuwavutia mashabiki, au pengine hana la kusema baada ya uongozi kushindwa kutimiza ahadi.
Ni wakati wa uongozi wa Simba SC kujitokeza na kusema ukweli kuhusu hatma ya klabu badala ya kuendelea kuwapa mashabiki ndoto ambazo haziishi kila msimu. Muda wa hadithi umekwisha, sasa mashabiki wanahitaji v
itendo.
Imeandikwa na NALIA NGWENA the ball dancer Pakome Zuzwaa.