Boss wa Simba SC Mo Dewji Bado Kimya, anatunga mbinu mpya ya Kuwadanganya Mashabiki

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
11,297
Reaction score
14,588
Msimu wa 2025/26 unakaribia kwa kuanza, lakini jambo la kushangaza ni ukimya wa mfadhili mkubwa wa Simba SC, Mohammed Dewji (Mo Dewji). Mashabiki wengi wa Simba wanajiuliza, ni kipi kipya Mo Dewji anakiandaa? Au bado anatafakari mbinu mpya ya kuwashawishi na kuwadanganya kuhusu mafanikio ya msimu ujao?

Msimu uliopita ulijaa ahadi kubwa kutoka kwa uongozi wa Simba, ikiwemo bajeti ya mabilioni ya shilingi na usajili wa wachezaji wa kiwango cha juu, lakini matokeo yalikuwa tofauti kabisa na matarajio ya mashabiki. Hadi sasa, hakuna kauli wala mwelekeo rasmi kutoka kwa Mo Dewji kuhusu maboresho ya timu wala mkakati wa msimu mpya.

Mashabiki wa Simba wanahitaji ukweli, siyo porojo na matumaini hewa kama ilivyokuwa misimu iliyopita. Ukimya wa Mo unaweza kuwa ni sehemu ya mkakati wa kutengeneza simulizi mpya ya kuwavutia mashabiki, au pengine hana la kusema baada ya uongozi kushindwa kutimiza ahadi.

Ni wakati wa uongozi wa Simba SC kujitokeza na kusema ukweli kuhusu hatma ya klabu badala ya kuendelea kuwapa mashabiki ndoto ambazo haziishi kila msimu. Muda wa hadithi umekwisha, sasa mashabiki wanahitaji v
itendo.

Imeandikwa na NALIA NGWENA the ball dancer Pakome Zuzwaa.

 
Timu ipo ya Tano ranking za vilabu Bora Barani Afrika.....! Kabla ilikuwa kama Yanga Hata 10 Bora ilikuwa haipo.

Unataka MO aseme nini Tena. Vitendo tu vinaongea.
 
Timu ipo ya Tano ranking za vilabu Bora Barani Afrika.....! Kabla ilikuwa kama Yanga Hata 10 Bora ilikuwa haipo.

Unataka MO aseme nini Tena. Vitendo tu vinaongea.
Anataka awafurahishe mashabiki. Anatamani timu ikusanye makombe ya ndani hata akiishia makundi timu iwe na mabakuli mengi yenye thamani ndogo kifedha ili mashabiki wafurahi. Mo anataka hela kwanza halafu ndani ya hizo pesa mashabiki wafurahi. Timu haina ufadhili wa chama, pesa inahitajika ili mfadhili afurahi na aweze furahisha mashabiki, pesa ya msimu nzuri ni ukivuka makundi club bingwa na kuendelea mbele, sio kukusanya tu mabakuli ya M100.
 
Timu ipo ya Tano ranking za vilabu Bora Barani Afrika.....! Kabla ilikuwa kama Yanga Hata 10 Bora ilikuwa haipo.

Unataka MO aseme nini Tena. Vitendo tu vinaongea.
Kwa hiyo tano Ranking ndiyo mafanikio ya msimu?!!!
 
Sisi mashabiki wa simba hatuna deni kwa tajiri yetu Mo, Mwenyekiti wetu Mangungu, wachezaji na benchi lote la ufundi likiongozwa na kocha wetu Fadlu Davis.
 
Ilituchukua miaka 59 (1961-2020) kujenga vituo 8,783 vya kutolea huduma za afya.

Mama ametumia miaka minne (2021-Aprili 2025) kujenga vituo 4,063.

Kwa miaka 10, atajenga vituo sawa na tulivyojenga tangu uhuru.

#TikiKwaSamia
 
Muheshimu hata kama Humpendi mkuu.

Hata mimi simkubali kuanzia Bilioni 20 aina yake ya uwekezaji, kususa susa nk Lakini siwezi kumvunjia heshima.

Heshima ni kitu cha Bure.
kwani unavyoona tusi lipo wapi
 
Ilituchukua miaka 59 (1961-2020) kujenga vituo 8,783 vya kutolea huduma za afya.

Mama ametumia miaka minne (2021-Aprili 2025) kujenga vituo 4,063.

Kwa miaka 10, atajenga vituo sawa na tulivyojenga tangu uhuru.

#TikiKwaSamiaView attachment 3396689
oya tugawane pesa basi tupushi agenda wote kuna akaunt zangu hazina cha kupost huko facebook
 
Amemsajili Jimmy Morred Morro kutoka Tukuyu Stars
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…