Boss wangu ananinyanyasa; Sheria ikoje?

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Wapendwa habarini za Leo?
Boss wangu ananisumbua kweli kweli yaani sina amani ya kazi hata kidogo, ni mwanamke na anatoka nchi jirani, nimejaribu kucheki ni wapi nimekosea but sioni. Anafikia kipindi cha kunitukana, yaani ile kunifokea haridhikli nayo sasa kaamua kabisa kunitukana anavyopenda, kumpiga natamani but sheria inasemaje? Naombeni mwenye uewelewa juu ya hili...

CC: MANI zumbemkuu Little Angel
 
Last edited by a moderator:
Najua muda si mrefu nitajiajiri mwenyewe lakini si hata mbuyu ulianza kama mchicha? Natamani sana sana nimalbue makofi
 
Umejaribu kuchunguza au kuhisi chanzo ni nini?
Ni aina gani ya kazi aliyokuajiri?
Una muda gani kazini,na manyanyaso yameanza lini(hivi karibuni au zamani)?
 
ukiona anakunyanyasa ujue wameshakuchoka au anafanya kusudi akijua huna pakwenda, onyesha msimamo sio siku zote uwe mpole kama kondoo, bosi wangu wa kwanza alikuwa mhindi, alichokipata hatosahau maisha yake yote....
 
Mpwa ni shirika tena la kimataifa sio Local, nina zaidi ya mwaka na nusu sasa, nina hisi ana mtu anataka kumweka kwenye post yangu so anachokifanya ni kuninyanyasa ili niwe frustrated niache kazi ....
Umejaribu kuchunguza au kuhisi chanzo ni nini?
Ni aina gani ya kazi aliyokuajiri?
Una muda gani kazini,na manyanyaso yameanza lini(hivi karibuni au zamani)?
 
watakuja wataalamu wakujibu, ila utaalamu wangu mimi naona bora upige makofi hadi alazwe, hazijui ngumi za Wa Tanganyika huyo
 

she could be in LOVE with you! inawezekana mwanzoni alijaribu kukuonyeshea vitabia fulani vya kike ili uelewe kuwa anakutaka kimapenzi ila wewe hukujua hizo signs! mwanamke anaweza akakutaka kimapenzi akajaribu kukuonyeshea signs...akiona husomeki huwa anageuka kuwa enermy kwako! na wengine huwa anam-treat mwanaume vibaya ili ampate kwenye anga za mapenzi! try this...siku moja vaa smartly nenda kazini. tafuta muda ambao atakuwa peke yake ofisini kwake...mgongee. ukiingia ndani umwambie sorry bosi naomba kuongea nawe. uso wako uwe mchangamfu na usio na tahayari. kisha kaa kwenye kiti huku ukimtizama usoni then mwambie..you are a very good boss. ila huwa sijisikii vizuri unavyonitukana. naomba uniambie kosa langu ili nijirekebishe maana mimi ni mwanadamu. naweza kukosea bila kujua. utamsikia anasema nini na mchunguze movements za mwili wake na the way she talk to you. hapo kama anakupenda kimapenzi utamgundua tu. baada ya wiki usipoona response yake like kukutaka taka hivi ujue ana mpango wa kutaka wewe uache kazi! mind you kama ataanza kukutoa lunch na kuku-approach kimapenzi mimi simo na sijakushauri um-date!
 
Kuwa mpole, halafu omba appointment ya kumuona, tena mcheki siku akiwa na mood nzuri ndio ufanye hivyo. Kisha akikubali nenda mwambie umekuja una shida unaomba akusaidie ni maeneo gani yeye anaona hufanyi kazi vizuri muombe akuelekeze na muahidi akikuelekeza hutamwangusha. Uzoefu wangu unaniambia tatizo lako (mtanisamehe) ni lile la vijana wa sasa wa ki TZ la kutotaka kufanya kazi kwa usahihi na weledi, kila kitu mpaka uambiwe, ubunifu hamna, uvivu. sasa kwa vile huyo katoka jirani(Kenya I guess), wenzetu hawana longolongo kazini. Na kama anakutaka angeshakuambia, kwa hiyo chapa kazi kijana utaona atakavyokupenda.
 
Hizi ajira za NGOs naza watu binafsi huwa huwa hazina guarantee, ukiona hivyo jipange maana upo karibu kufukuzwa. Hakuna haja yakugombana ila tafuta njia yakumuambia kuwa wewe siye mtoto wake hivyo aache kukutukana kama mtoto mdogo.
 
Mpwa ni shirika tena la kimataifa sio Local, nina zaidi ya mwaka na nusu sasa, nina hisi ana mtu anataka kumweka kwenye post yangu so anachokifanya ni kuninyanyasa ili niwe frustrated niache kazi ....
Nakushauri,
kwanza-zingatia majukumu yako kwa sasa,timiza wajibu wako ipasavyo kama inavyoelekezwa kwenye mkataba wako wa kazi.
Pili-Ondoa fikra za kuwa anakufanyia visa ili uondoke aweke mtu mwingine(yeye ni muajiri nadhani anajua hatua za kisheria za kukuachisha kazi wakati wowote atakapo hata kuweka mtu mwingine anaweza pasipo kukuletea kelele) jaribu kustay positive.
Tatu-Kuhusu matusi na kufoka pasipo mpango,kutana naye uso kwa uso na umweleze kuwa afanyalo si sahihi na hufurahii tabia hiyo na kama kuna jambo akueleze kiungwana si vinginevyo
Hitimisho:kama haya kati ya jitihada nyingine zitashindikana,basi rejea kwenye mkataba wako wa kazi wapi ulielekeza iwapo itatokea umetofautiana na mwajiri wako (bodi ya usuluhishi,mahakama n.k)

JARIBU KUSULUHISHA KIMAKUBALIANO KATI YAKO NA MWAJIRI KABLA YA KUPELEKA KWENYE SHERIA(TETETEA KIBARUA CHAKO)
 
Hizi ajira za NGOs naza watu binafsi huwa huwa hazina guarantee, ukiona hivyo jipange maana upo karibu kufukuzwa. Hakuna haja yakugombana ila tafuta njia yakumuambia kuwa wewe siye mtoto wake hivyo aache kukutukana kama mtoto mdogo.

Haswaaaaaaaa,Ngo's ndo wanataka uwalambe miguu ,mi nlishamtukana secretary anataka nimlambe miguu kisa ana urafiki na one of Board memberz..nkamtukana hadi akawa na heshima na adabu na nilijua next habar zitafika kwa Board na mkataba hautakuwa renewed..ndivyo ilvyotokea..lakin aaah naish mjini na Muhuri wangu wa uwakil..Inafika wakati lazma ufanye maamuz magumu si kukubali kutukanwa..hata watoto zetu tunawapa nafasi ya kujieleza si kuvamia tu na kugombeza ebo!!
 
Anakupenda jaribu kumtongoza uone,

just kidding (soorrry)
ndo maana ninang'ang'ania govt ingawa kamshahara sisimizi, yaan full kujaichia
 
The legal provisions are very clear in that the Employment and labour Relation prohibits employers to discriminate directly or indirectly against an employeein any employment policy or practice on grounds of colour; nationality; tribeor place of origin; political opinion or religion, sex, gender, pregnancy,marital status or family responsibility, disability, HIV/AIDS; age or station oflife.Also it prohibits harassment of employees on any one or combination of the grounds.Your case is simply a harrassmentand can be initially be dealt with at work place.Now do you have a grievance procedure that you can use to lodge your claim?.If there is good grievance procedure use it and in case it fails you may forward your matter to Commission of Mediation and of Arbitration .The good thing about cases of discrimination and harrassment is that the law has criminalized it and therefore employers can be taken to court if they dont deal properly with case of discrimination.As these cases can be tricky in practice I advise you to see the HR Manager for advice.
 
Thank you Mpwa, Togoloa Mosie
 

Hii habari yako inamapungufu maana unalaumu tu lakini hutuambii chanzo ni nini,inawezekana kwa unayoyafanya unastahili kufukuzwa kabisa lakini akiiwaza familia hiyo ndio option anayobakia nayo,so tuambie vizuri kulikon?
 
Mpwa sina chanzo na naamini hakuwezi kuwa na chanzo kwa upande wangu, aligeuka tu ghafla na kuanza kuninyanyasa
Hii habari yako inamapungufu maana unalaumu tu lakini hutuambii chanzo ni nini,inawezekana kwa unayoyafanya unastahili kufukuzwa kabisa lakini akiiwaza familia hiyo ndio option anayobakia nayo,so tuambie vizuri kulikon?
 
Kuna kitu usichokujua kinaendelea hapo kazini
Endelea kuwa imara mda si mrefu utakijua na kufanya uwmuzi wa maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…