BOT imepanga Kushirikisha vyuo vikuu ukuzaji wa akili Unde

BOT imepanga Kushirikisha vyuo vikuu ukuzaji wa akili Unde

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) leo tarehe 22 Januari 2026 imesaini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano (MoUs) na taasisi tano za elimu ya juu kwa lengo la kukuza matumizi ya akili unde (AI), kuimarisha ubunifu katika matumizi ya data, na utafiti katika kuongeza tija kwenye uundaji wa sera na usimamizi wa sekta ya fedha, Alieleza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.

Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Chuo Cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika (EASTC), Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Bw. Tutuba ameongeza kuwa utekelezaji wa makubaliano haya unaoana na malengo ya Dira ya Maendeleoya ya Taifa 2050 ambapo ukuaji wa teknolojia ya kidigitali ni kiwezeshi kimojawapo katika utekelezaji wa masuala mbalimbali ya kiuchumi.

“Tunapoongelea kuwa na taifa litakalokuwa na uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050, kuna mchango mkubwa sana wa masuala ya Akili Unde, ubunifu wa matumizi ya data na matumizi ya mifumo ya kidijitali”, amesema Gavana Tutuba.

Aidha, ameeleza kuwa vyuo ambavyo Benki Kuu imeingia navyo makubaliano hayo vimeonesha umahiri katika kuendesha mafunzo mbalimbali kwa ngazi ya Shahada na Shahada ya Uzamili na vinavituo maalum vya AI na ubunifu katika matumizi ya Data.

“Vyuo hivi vimekuwa mahiri sana katika kuendesha mafunzo katika ngazi ya Shahada na Uzamili na wote wamekuwa wakifanya vizuri katika masuala ya teknolojia ya kisasa yanayohusisha Akili Unde na Ubunifu wa matumizi ya Data”

Makubaliano haya yanahusisha Itifaki ya Ushirikishwaji wa Data (Data Sharing Protocols) na yanazingatia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Data Protection Act) , ambapo BoT itatoa data zilizozingatia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Data Protection Act).

Itifaki hizi zitawawezesha watafiti vyuoni kupata uzoefu wa kutatua changamoto halisi, kupunguza muda wa utafiti unaosababishwa na ukosefu wa data, na kukuza ubunifu katika akili unde na matumizi ya teknolojia za kisasa za data
 
Back
Top Bottom