BoT inakuja dawa ya wakopaji "makanjanja".

BoT inakuja dawa ya wakopaji "makanjanja".

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,112
Reaction score
4,540
Serikali imeanzisha mfumo wa kuweka
rekodi za wakopaji wa taasisi za fedha
ili kudhibiti upotevu wa mikopo kupitia
wateja wasio waaminifu.
Pia mfumo huo utasaidia kupunguza
masharti ya ukopaji ikiwemo utozaji wa riba kubwa.
Mfumo huo wa kukusanya na
kushirikishana taarifa na kumbukumbu
za wakopaji wa benki na taasisi za
mikopo midogo, ulizunduliwa jana Dar es
Salaam na Benki Kuu (BoT), ambayo ndiyo itakayousimamia na kuufuatilia.
Naibu Gavana wa BoT, Juma Reli,
alizinduzi mfumo huo na kusema
utasaidia kupata taarifa za wakopaji
ambazo awali kukosekana kwake
kulisababisha wateja wengi kukosa mikopo na pia kulazimisha vyombo vya
fedha kuweka viwango vya juu vya riba.
Reli alisema “kukosekana kwa taarifa za
mkopaji na mwenendo wake wa kulipa
deni kumesababisha benki zishindwe
kutoa maamuzi sahihi ya kukopesha ama kutokukopesha wateja”.

Hatua ya BoT imekuja wakati Tanzania
ina mabenki ya biashara zaidi ya 49
ambayo hutoa mikopa kwa wateja
mbalimbali ambao taarifa na
kumbukumbu za uadilifu wao kwenye kulipa madeni zilikuwa hazijulikani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Usimamizi wa Benki wa BoT, Agapiti
Kobello , akizungumzia mfumo huo
alisema benki za biashara na taasisi
wakopeshaji zinawajibika kisheria kuwasilisha taarifa za wakopaji wao BoT
ili kuwezesha ushirikishanaji na utoaji
wa taarifa hizo kwa wadau wengine.
Alisema lengo la kuanzisha mfumo huo ni
kujenga uwajibikaji wa ulipaji mikopo
na pia kuwawezesha wakopeshaji kuangalia historia za wateja na kupata
taarifa sahihi za wateja waaaminifu na
‘matapeli’.

Alisema benki hiyo ilitumia mkandarasa
kuandaa mfumo huo ambao ulifanya
majaribio ya benki 26 na kati ya hizo tisa zimewasilisha taarifa za wakopaji wake
BoT na kusisitiza kuwa benki nyingine
zinapewa mwezi mmoja kuwasilisha
taarifa zao na zikishindwa hatua za
kisheria zitafuata.
Mfumo huo wa kukusanya na kushirikishaana takwimu mkeka
(database) na kumbukumbu za wakopaji
utatafuta taarifa za wakopaji kupitia
makampuni ya simu, mashirika
yanayotoa huduma kama TANESCO,
wakala na mamlaka za serikali zinazoshughulikia vitambulisho , pasi za
kusafiria, kusajili biashara na ripoti za
mahakama.

Katika uzinduzi huo, Miguel Llenas
mwakilishi wa kampuni binafsi ya Dun &
Bradstreet Credit Bureau Tanzania, iliyopewa kibali na BoT cha kukusanya
takwimu mkeka za wakopaji,
alizungumzia mafanikio ya mfumo huo
yaliyopatikana nchini za Amerika Kusini.
Alisema umewezesha taasisi za fedha
kukusanya madeni kwa uhakika, kujua taarifa za wakopaji na wakopeshaji na
kufahamu rekodi na mwenendo wa
wateja mbalimbali na tabia zao za kulipa
madeni. CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom