BoT: Pesa ya Tanzania haiwezi kusambaza Virusi vya Corona. Zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti

Waache iingie uswahilini, Tandale, Mbagala, Buguruni au Gongolamboto huko ndipo akili itawakaa sawa!

Haitaweza kudhibitika tena, maafa yake yatakuwa afadhali ya vita!

Kipindupindu tu kinawatesa kuondoa ngoja tuone
Corona ikilipuka uswahilini lockdown is not an option kudhibiti maambukizo zaidi-utauawa watu kwa njaa .
 
Sasa naanza kupata hisia kwamba hata yule Isabella Mwampamba huenda ni mchongo uliochongwa na serikali ajitangaze kwamba ana Corona halafu ionekane pamoja na kuwa na Corona lakini si tishio kwasababu pamoja na kuwa na maambukizi lakini haumwi chochote kile.
Yote hayo ni ili kuondoa Panic.

Eitherway, ugonjwa huu umekuzwa sana na ni matokeo ya kila mtu kumiliki 'chombo' cha habari.
View attachment 1392836
Benki Kuu ya Tanzania imesema noti za Tanzania zimetengenezwa kwa namna ambayo haziwezi kuhifadhi virusi.
 
Kutoa hofu tu. Ukishatumia neno... hata hivyo…. basi umemaliza, wenye kuelewa wamelewa.
 
Hapa BOT wangepotezea tu. Hakukuwa na sababu ya kuandika haya.
 
Hata mimi naamini huyu Esabella siyo mgonjwa ila mla bata tu aliyetafutwa kwa kazi maalumu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inapaswa kufungulia simu zote ambazo hazijakamilisha usajili kwa alama za vidole ili kupunguza kasi ya maambukizo kutokana na matumizi ya noti. Tuache uzembe corona is highly contagious.
Pia wailazimishe mitandao ya simu ipunguze makato mtu anapofanya miamala.

Kwa kuanzia wangeweka kiwango cha juu cha kufanya muamala isizidi sh. 1000 hasa kwenye kutoa. Kama mtu anafanya muamala wa chini ya elfu hamsini iwe bure.

Wakiweza hili nadhani idadi kubwa ya watanzania hata soda watanunua kwa mpesa. Itasaidia sana katika kipindi hiki kigumu.
 
BOT wamekuwa wataalam wa afya ..enhee
Wataalam wa afya wa South Korea na China waligundua Corona virus alikuwa anasambazwa na cash kwa hiyo waliamua kuchukua hatua ya sanitization of bank notes and coins.
Na maambukizi yao yameshuka mno.

Sisi huku ni ujuaji hata kabla ya tafiti ndogo tu ya kisayansi.
Tafiti za mwanzo zinaonyesha Corona virus anaweza kusurvive nje ya mwili wa binadamu hata kwa siku tatu, sasa noti na coins za hii donor country yetu zina ubora gani wa ajabu kushinda nchi zenye uchumi mkubwa kama South korea.

Ujuaji mwingi maarifa hakuna.
 
Hata mimi naamini huyu Esabella siyo mgonjwa ila mla bata tu aliyetafutwa kwa kazi maalumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee kuna uwezekano huo. Zile drama za jana za kumpigia simu live halafu akaanza blah blah za kuomba msamaha na kuishukuru serikali ya rais nani sijui...Nikajua hapa mh..maigizo mengine haya. Ikumbukwe ni kinyume cha maadili kuanika hadharani jina la mgonjwa na ugonjwa anaogua.
 
Ugonjwa huu upo ,denial haiwezi kutusaidia kuepukana na maafa . Zaidi ya watu 400 wamefariki jana(hesabu ya siku) Italy.
 
Kwa hiyo noti zetu zinatibu corona

Sasa kumbe dunia inahangaika na dawa ya corona kumbe dawa ipo huku Tz kwenye noti Dadeek walah
@ Trump
@ Xi

Mkuje huku Tz mchukue minoti yetu inatibu corona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…