Wan JF.
Msipoamini habari nilizoandika kuhusu poision aliopewa huyu bwana balali hiyo ni shauri yenu. Lakini ukweli uko pale pale na ndio hicho kilichotokea.Aliyenipa hizi habari ni mwanafamilia wa Balali na unajua tena hawezi wenda indeep more that that maana naye hajui kama mimi nilikuwa namchota ili nilete habari au la! Lakini kwa kuwa ninaishi hapa na nimejiahidi kuyasaka yale nayoweza kuyapata kutoka kwa ndugu wa balali aliyeko hapo. Lakini tatizo la JF kuna ka-tabi ka kudhalilishana. Ukiniuliza maswali eti kwa nini hawakumpa maziwa mara baada ya kugundua amepewa sumu...sasa mimi unataka nikujibu nini. Ninachojua ni kwamba hiyo sumu iliharibu sehemu za utumbo wako kama nilivyoeleza ndio maana akafanyiwa operashion. Tuwe tunaheshimu mchango wa mawazo ya wenzetu kuliko kukandia na kuingiza ukabila kwa waota habari kama baadhi ya memmbers hapa mlivyonishambulia. Ukweli utakuja julikana na mimi naamini nilichokisema kitaibuka kuwa cha kweli na hakuna yeyote hapa atakayekubali kwamba nilishakisema. Mimi nitaendelea kudondosha habari kila nitakavyozipata.
"BALALI YUKO KWENYEHOTEL NDOGO YA MTAANI NA SI RAHISI KUMPATA KWASABABU HOTEL HIYO SI POPULAR SANA" hayo ni kati ya niliyoyataja kwenye thread yangu ya awali na yametoka kwa huyo mwanafamilia wake. Tuache ubishi usio na sababu bali tudadisi.
Nshomile,
Nina wasiwasi sana na maneno uliyoambiwa. Unajua suala la Ballali kuna spinning nyingi sana lakini wakati mwingine ni rahisi kuondoa spinning kutoka kwenye facts kwa kuangalia utendaji wa huku.
Ballali yuko USA, kama sumu ilitumika kumuunguza, hospitali yoyote alikoenda, kitu cha kwanza watatoa report polisi. Huo ni uhalifu na Dr.
yeyote huku magharibi akiona kitu kama hicho, anatakiwa kutoa taarifa polisi.
Nitashangaa kweli kwa USA kama itaonekana Ballali kapewa sumu na vyombo vya dola visiingilie, nitashangaa sana.
Huenda wanaotoa uvumi kama huo hawajui jinsi hospitali huku nje zinavyofanya kazi.
Hivi hapa hatuna madaktari ambao wanafanya kazi Europe au USA ambao wanaweza kutusaidia ku clarify juu ya hili?
Mimi ninachohisi ni kwamba Ballali anahusika kwenye wizi huo, ameshirikiana na watu wakubwa serikalini, wamemficha USA kwa faida yake yeye Ballali na hao watu wa serikali. Watajaribu kumtoa yeye kafara lakini hawatamtafuta kutaka arudi nyumbani.
Kuna ndugu wa Ballali wako hapa na laiti ingelikuwa issue ni sumu, ungesikia cheche ambavyo zingemwagwa. Naamini hakuna ukweli, hata wanaosema hayo ni kutaka kumlinda ndugu yao.
Walikuwa na uwezo wa kuitoa barua yake ya kujiuzulu, wakitegemea itasaidia kuondoa balaa la kufukuzwa kazi. Sasa naona wanaanza spinjing zingine.
Ballali inatakiwa afanye alicho fanya Marion Jones, atoke clean hata kama
itamfanye aadhibiwe. Waliosema "If you are in a hole, stop digging" hawakukosea. Usanii unaoendelea sasa huenda ukamletea matatizo zaidi huko mbele.