na sasa Balali....the list is endless.
Wakuu Mwanakijiji, na Jasusi, endeleeni kutupa dataz hatuhitaji Death Certificate ili kuwaamini kuhusu yanayojiri na Gavana Balali,
hawa wakuu kuna wakati walituletea dataz za Mungai kuwa Waziri Mkuu na kwamba ameshapewa watu wa usalama wa kumlinda imebakia kutangazwa tu, sasa hao hao tena wanadai Death Certificate ili wasiamini kwamba Kombe mkuu wa Intelligence ya Jamhuri, kuuwawa kwake kwa kupigwa risasi na local police eti kwa kumfananisha na jambazi aliyekuwa akitafutwa huko kitongojini, ilikuwa ni Kolimbad style!
Hivi mtu mwenye position kama yake si huwa anafuatana na bodyguards, tena wengi sio mmoja na ni lazima afuatane na magari angalau mawili, na hata mahakama yetu bongo sio ya the Haque ilikubali kuwa kulikuwa na faulo na ikaamuru familia yake ilipwe karibu Shillingi Millioni 400, lakini kuna wanaotaka tuwaletee Death Certificate ambayo hata hakimu hakuihitaji katika kuamua kesi hiyo ya Wrongful Death mikononi mwa serikali,
Jasusi na Mwanakijiji tupeni dataz za ex-Gavana, tunazifuatilia kwa makini, na JF idumu maana hapa ndio mwanzo na mwisho wa dataz, hata Mwana-Halisi sasa huja hapa kutafuta dataz, uliza gazeti lao la juzi lilivyojaaa topic moja ya hapa ya "watoto wa Vigogo na BOT", na "NY", yaani wewe viongozi wanagawana nchi na kuchezeana akili, wewe unauliza Death Certificate?
Eti unataka Death Certificate ya RIP Amina Chifupa?
JF yaani idumu tu na kumkoma nyani mbele, huwa hatuangalii usoni!