BoT watoa scholarships kwa undergraduate & postgraduate 2014/2015

Brother James

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
233
Reaction score
172
Kwa heshima ya Mwl. Nyerere, Benki Kuu ya Tanzania(BOT) wametoa fursa kwa watanzania wanne (4) kwa ngazi ya undergraduate na watanzania wawili (2) kwa ngazi ya postgraduate/Masters kuwasomesha bure (scholarships) endapo watakidhi vigezo walivyoweka. Scholarships hizi wamezipa jina la Mwl. Julius K. Nyerere Memorial Scholarship Fund.

Deadline ya kuomba kwa undergraduate ni tarehe 12/09/2014 na deadline kwa postgraduate ni 29/10/2014

KWA MAELEZO YA KINA JUU YA SCHOLARSHIPS HIZI SOMA HAPO CHINI. VIAMBATISHO(ATTACHMENTS) ZA UJUMBE HUU NI FORMS ZA KUOMBEA SCHOLARSHIPS HIZI PAMOJA NA RECOMMENDATION FORM kwa ajili ya waombaji wa Postgraduate. NIWATAKIE MAFANIKIO MEMA WOTE WENYE SIFA:

UTANGULIZI:

Scholarships hizi kwa mara ya kwanza zimetolewa mwaka wa masomo 2013/2014 na walengwa walikuwa ni wasichana waliofanya vizuri (A-Level) katika masomo ya sayansi na Hisabati kupewa fursa ya kusomeshwa bure (kwenye fani za sayansi na hisabati) katika vyuo vikuu vya kitanzania na kulipwa fedha za chakula ma malazi pamoja na laptop moja kwa kila scholar. Pia walifikiria kutoa ufadhili mdogo kwa wanafunzi watakao soma fani za Economics,IT, Accounting & Finance. Pia wakafikiria kutoa ufadhili kwa level ya Masters katika fani tajwa hapo juu japo kwa uchache.

LENGO KUU LA UFADHILI/SCHOLARSHIP

BOT wamenuia kuwainua kielimu wanawake hususani katika masomo ya sayansi na Hisabati husasani katika ngazi ya Shahada/degree na Shahada ya Uzamili/Master na kwa uchache kutoa motisha kwa wanaume wachache waliofanya vizuri zaidi katika masomo/fani tajwa. Scholarships hizi hufadhili malipo yote yahusuyo gharama za kielimu kwa mtu aliyepewa ufadhili huu ikiwa ni pamoja na gharama za udahili wa chuoni, chakula, malazi, practicals, ada, laptop moja, na gharama nyinginezo zoote.

MGAWANYO WA UFADHILI HUU


1.UNDERGRADUATE:

(i) Scholarship mbili (2) ni kwa wadada waliofaulu vizuri (A-level) katika masomo ya sayansi na Hisabati na ambao
wamejiandaa kusomea masomo ya sayansi na Hisabati ngazi ya degree

(ii) Scholarship mbili (2) ni kwa ajili ya wavulana na wasichana waliofanya vizuri katika masomo yao ya A-level na
wana sifa za kujiunga katika vyuo vikuu kusoma fani za Economics, Accounting, Finance na IT.

SIFA ZA WAOMBAJI WA (i)

a. Wawe watanzania waliohitimu A-level mwaka 2014 na wenye ufaulu wa daraja la kwanza na wapate alama "A'
katika somo moja wapo kati ya Hisabati na Sayansi (Chemistry, Physics, Biology)

b. Wawe na ufaulu mzuri katika cheti cha O-level na wawe wameomba/dahiliwa katika vyuo vikuu vya Tanzania kwa
mwaka wa masomo 2014/15 hususani ktk fani za Hisabati na sayansi tu.

SIFA ZA WAOMBAJI WA (ii)

a. Wawe watanzania waliohitimu A-level mwaka 2014 na wenye ufaulu wa daraja la kwanza na wapate alama "A'
katika somo moja wapo kati ya Hisabati, Commerce, Economics, Acounting na Sayansi (Chemistry, Physics, Biology)

b. Wawe na ufaulu mzuri katika cheti cha O-level na wawe wameomba/dahiliwa katika vyuo vikuu vya Tanzania kwa
mwaka wa masomo 2014/15 hususani ktk fani za IT, Economics, Accounting & Finance

2. POSTGRADUATE/MASTERS

i. Ngazi hii, waombaji wote (wanaume na wanawake) wanasifa za kuomba ufadhili bora wawe watanzania tu

ii. Waombaji wote wawe na first class na upper second class wenye ufaulu wa chini kabisa 4.0 GPA katika degree zao wa kwanza na wawe wamehitimu kati ya mwaka 2013 na 2014 tu.

iii. Waombaji wawe wamedahiliwa kusoma katika vyuo vikuu vya nchini Tanzania na wawe wamedahiliwa kusomea fani zifuatazo; IT, Mathematucs, Science, Economics & Acconting.

JINSI YA KUOMBA UFADHILI


i. Form za kuombea zinapatikana kwenye website hii: Bank of Tanzania (BOT): Home Page : Benki Kuu ya Tanzania (nime iambatanisha kwenye ujumbe huu)

ii. Ukisha ijaza itume kwenye anuani ifuatayo:

THE CHAIRPERSON
SCHOLARSHIP AWARD COMMITTEE
MWL. JULIUS K. NYERERE MEMORIAL SCHOLARSHIP FUND
BANK OF TANZANIA
2 MIRAMBO STREET
P.O. BOX 11884
DAR ES SALAAM

*****MWISHO
 

Attachments

Huu ni wehu sasa kwahiyo wanafunzi wote wasome sayansi au sio?
 
hz GPA mbona kubwa sana?
Mgumu04, mara nyingi scholarships nyingi duniani hutolewa kwa watu ambao ni very exceptional/genius ambao wameonyesha uwezo wao wa ziada katika taaluma na ufaulu, watu wa aina hii ni wachache na ndio maana fursa za scholarships pia huwa ni chache li zitumike kama motisha kwa watu walio-strugle hard ktk taaluma
 
BIGURUBE, umeonyesha in-born character yako ya uchoyo kwa kutotoa taarifa kwa wadau wa JF juu ya uwepo wa scholarships za aina hii, Umeona mambo yapo hadharani ukaamua kuonyesha kuwa umepata taarifa mapema zaidi yetu (yawezekana kweli/si kweli).
Ungekuwa na mshipa wa aibu wala usingetamka kitu kama hiki hapa JF coz mimi naamini kuwa taarifa zozote muhimu huwa tunapeana tena kupitia hapa JF ili kila mtu aone umuhimu wa kuwa member wa JF.
Nitoe ombi kwa wana JF wote kuwa tusaidiane kupashana habari za muhimu kupitia kurasa za JF kwani si watu wote wepesi wa kutembelea tovuti mbali mbali ila JF ni kilinge chao cha taarifa.
Mwisho niseme kuwa thread ya aina hii ni ya kwanza kuingia hapa JF hivyo basi wote tuamini kuwa habari hii ni ya leo leo wala si kama alivyosema BIGURUBE.
Watu kumbe mnachelewa sn kupata habari, hii issue INA zaidi ya 2weeks
 
Shardcole, frankly speaking mahitaji ya serikali kwa sasa ni wataalam katika fani za Sayansi, pia taasisi (BOT) inayotoa ufadhili huu inahusiana kabisa na masuala ya fani walizozitaja, pole sana kama umekosa sifa kwenye ufadhili huu

Pamoja na usawa wa Kijinsia mbona wadogo zetu wakiume wametoswa? Si inaonekana wanaume na wanawake wote ni sawa, mbona hapa BOT wamewapa promo dadaz pekee
 
Well, nimekuelewa vizuri sana CHAZA, kwa sasa serikali inawa-empower women ili angalau idadi yao ilingane lingane na idadi ya wanaume hususani kwenye suala la kielimu na kimadaraka. Ni kweli na wazi kabisa kuwa taasisi nyeti za umma zimekuwa na kasumba ya kuwabeba ladies ila kwa mfano wa pale BOT men ni wengi sana tena ni top officials ukilinganisha na wadada wachache wanaofanya kazi pale, vivyo hivyo kwa Idara/Taasisi nyinginezo, therefore upendeleo unaofanywa wa kuwabeba ladies ni wa kimkataba, serikali inatambua fika japo kuna taasisi hawafuati utaratibu uliowekwa na serikali ktk kuwa-empower women.
Pamoja na usawa wa Kijinsia mbona wadogo zetu wakiume wametoswa? Si inaonekana wanaume na wanawake wote ni sawa, mbona hapa BOT wamewapa promo dadaz pekee
 
Well said Brother James, tunataka taarifa na sio bra bra tu....you did a good job for sure
 

Nmekusoma kaka. Kwa kuwa ni dada zetu wacha nao wapate fursa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…