Boti yalipuka

Boti yalipuka

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Posts
4,201
Reaction score
236
Tumepata habari kuwa kuna boti toka tanga kwenda pemba imelipuka/imewaka moto leo alfajiri imeua watu 70
 
Mh imeua watu 70? Mbona habari zinatatanisha? Nway poleni wahanga wa boti hiyo.
 
Mod's hii iwekwe kwenye habari mchanganyiko.
Shy tupe more details.....
 
Mod's hii iwekwe kwenye habari mchanganyiko.
Shy tupe more details.....
 
Shy!

Hiyo habari ni muhimu kuijua ila naomba tupatie habari kamili tafadhali!..Ukiipata yote ongezea hapo!
Inasikitisha kama tukio hilo limetokea!..
 
Tumepata habari kuwa kuna boti toka tanga kwenda pemba imelipuka/imewaka moto leo alfajiri imeua watu 70

source?
kama imelipukia katikati ya bahari nani aliyeleta taarifa, then kuna uokoaji wowote? majeruhi watazikwa wapi?
Kama ni kweli biti imelipuka (hitilafu au ugaidi) natoa mkono wa pole kwa waathirika na walionusurika wapate nafuu mapema huku waliopoteza wapendwa wapate faraja kwa Mola
 
Hiyo ni boti ya kibiashara au boti-mtumbwi au ni mashua za waswahili!!???? Au isijekuwa ma-suicide bombers wako mazoezini!!!

Anyway, pole kwa wafiwa.
 
Last edited:
Taarifa zilizopatikana sasa hivi kutoka polisi tanga ni kuwa waliokufa idadi yao inakadiriwa kufikia 20. Watu 13 wameokolewa so far
 
Boti yenye jina Amana Pemba, ilikuwa na mizigo na abiria kama 40 hivi. Inaaminika kuwa moto ulianza kuunguza magodoro na kudakia kwenye mizigo mingine
 
Tushikamane kuwaombea majeruhi na wafiwa

Ni vema sana. lakini wakati tukiomba, nadhani umefika wakati wa kuwa na tafakuri ya kina, itakayotusaidia kuwa na mipango na kuepukana na ajali hizi au kuwa na mipango ya kukabilina nazo pale zitakapotokea.
 
source?
kama imelipukia katikati ya bahari nani aliyeleta taarifa, then kuna uokoaji wowote? majeruhi watazikwa wapi?Kama ni kweli biti imelipuka (hitilafu au ugaidi) natoa mkono wa pole kwa waathirika na walionusurika wapate nafuu mapema huku waliopoteza wapendwa wapate faraja kwa Mola

Msanii majeruhi hawazikwi mkuu.

Imelipuka bada ya injini yake kupata moto na kuunguza magodoro yaliyokuwa yamewekwa karibu na injini hizo. Ni kutoka Breaking news ya Radio One mchana huu
 
Hiyo ni boti ya kibiashara au boti-mtumbwi au ni mashua za waswahili!!????

Anyway, pole kwa wafiwa.

Inaelekea ni ya kibiashara kwa sababu ipo pia inayoitwa Amana Tanga ambayo inamilikiwa na mmiliki wa Amana Pemba. Kwa bahati nzuri, wakati ajali inatokea, Amana Tanga ilikuwa karibu na eneo hilo ikitokea Pemba kuelekea Tanga na ndio walisaidia kuwaokoa hao watu 13 (wafanyakazi saba na abiria sita ambao wamelazwa Bombo
 
Mungu tusaidie ajali hizi mpaka lini?
Marehemu wapumnzike kwa amani na tunawaombea majeruhi.
 
Pole kwa wafiwa!

Pemba usafiri wake wa maji sio mzuri hata kidogo! Kama kungekuwa na biashara nzuri nadhani wafanya biashara wangeweka boti za kasi! Lakini kwa sababu msukumo wa biashara ni haba na mchanganyiko wa siasa zetu ni vyema dola ifikirie jinsi ya kutatua maswala ya usafiri pemba!
 
Tumepata habari kuwa kuna boti toka tanga kwenda pemba imelipuka/imewaka moto leo alfajiri imeua watu 70

Duh! Hii inatisha!! Hivyo viboat sidhni hata kama vinafanyiwa maintenance bali ni kuwekwa baharini na kuhakikisha wanakusanya michuzi kadri wanavyoweza. Watu sasa Zenj itakuwa kwa ndege tu. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
 
Back
Top Bottom