Boti za Azam ni nzuri kwa huduma, wabadilishe na bendera

julaibibi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
3,081
Reaction score
4,224
Jana nimebahatika kufika visiwani kwa tamasha la idhaa za Kiswahili.

Azam ni wazuri kwa huduma hongera sana. Kitu moja sijapenda bendera ya taifa imechakaa sana . Nendeni GPSA zipo zinauzwa.

Bendera iheshimiwe hii inawakilisha mahali palipo na giza kama mwenge wetu tunu ya Taifa


 
Natumaini hata wewe umeliona hili na sio Taasisi binafsi tu hata taasisi za kiserikali pia hili tatizo lipo..... [emoji119].
 
Bendera inachangiaje wewe kufika mapema na kupata huduma nzuri? Sie ma carebean sealers kwanza boat au meli inapokuwa na bendera imechakaa manaake imekula upepo na mawimbi mengi baharini na ndio ufalme wa bahari huo
 
Si nilisikia mpaka iishe kabisa? Sema sisi ndiyo tunashobokea sana bendera. Wenzetu wanatundika majumbani mwao na popote
 
Hamna kitu zanzibar first ferry ukipanda hata ukimwambia mtu nipo kwenye ndege anakubali sema bakhresa kashawaroga hamsikii la mnadi swala wala mswalie mtume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…