Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Nchi ya Botswana inatarajia kuanzisha kituo cha kufanya ithibati ya almasi zinazouzwa kwenye nchi za G7 ifikapo mwakani 2025.
Hii inakuja kutokana na hatua ya nchi za G7 kuamua kutonunua almasi kutoka Urusi.
Kutokana na katazo hilo, kila almasi inayonunuliwa na nchi za G7 itatakiwa kufanyiwa ithibati kuthibitisha kuwa sio almasi inayotoka Urusi.
Kwa sasa kituo pekee cha kufanyia ithibati kinapatikana Antwerp nchini Ubelgiji.
Kituo cha kufanyia Ithibati cha Botswana pia kitatumiwa na nchi za Angola na Namibia.
Tayari nchi ya Namibia imetoa kauli ya kuunga mkono uanzishwaji wa kituo hicho.
CHANZO/ SOURCE : The North Africa Post.