"Bottom Up" Yamtokea puani William Rutto

KAMUKUNJI patakuwa mitaa kishua hapo!
 
Bottom up.... Hakumaanisha mipododo juu..... Hawa wakenya hawashindwi kuendeleza uwakala wao wa mambo ya ajabu..... Acha nkazimue konyagi😁😁

Haya wanyonge wekeni bottom up
 
Odinga hakushindwa kisa magufuli. Siasa za watu hauziwezi. Ni sawa na kusema umepigwa na laana ya magufuli kwa kupoteza biashara yako malawi
Masahihisho - Sijapoteza biashara yangu Malawi , nimepata hasara tu
 
Uhuru alisema Ruto ameshinda uchaguzi ila Rais wake ni Raila. Hii sentesi inafikirisha sana
 
Kwasasa ni raia mwema hivyo amedanganya akiwa serikalini Sasa anaendelea kuhadaa azimio akiwa uraiani
 
Wakati wa vuguvugu la uchaguzi wa Kenya, hadi wakati wa kampeni za uchaguzi huo, Dr William Rutto alitangaza mkakati wake kabambe wa kuwakwamua Wakenya kuagana na umasikini, ulioitwa Bottom Up, akimaanisha kuwakwamua kiuchumi Wakenya makapuku (kwa Tanzania wanaitwa wanyonge) na kuwapandisha kwenye hali nzuri.

Baadhi ya Wakenya wakamuamini na kuachana na Raila Odinga, ambaye alikuwa na nafasi kubwa ya ushindi kabla ya kutafunwa na laana kutokana na kuunga mkono udikteta wa serikali ya kikatili ya Tanzania iliyoongozwa na John Magufuli.

Cha kushangaza sasa baada ya Rutto kupata urais, akasahau haraka sana mkakati wake kwenye Bottom Up mithili ya mtu aliyelogwa ili asahau kwao, akaanza kuondoa ruzuku zilizowekwa na watangulizi wake ili kudhibiti bei ya mafuta, akidai anabana matumizi, utadhani hela za Kenya ni mali ya baba yake, bei ya mafuta ikainuka na hatimaye ikainua na bei za vitu vingine na kusababisha ugumu wa maisha ambao haukuwahi kuwepo tangu Yesu alipoondoka Galilaya.

Sasa Wakenya wamekiwasha mitaani wanataka kumng'oa.

Mungu ibariki Jamhuri ya Watu wa Kenya.
Wataweza kweli? Lakini wale hawaogopi kufa, usipo ogopa kufa unaweza kila kitu. Ukisha ogopa kufa kama watanzania tulivyo, basi.. huwezi lolote kwa siasa za afrika.
 
Wakati wa vuguvugu la uchaguzi wa Kenya, hadi wakati wa kampeni za uchaguzi huo, Dr William Rutto alitangaza mkakati wake kabambe wa kuwakwamua Wakenya kuagana na umasikini, ulioitwa Bottom Up, akimaanisha kuwakwamua kiuchumi Wakenya makapuku (kwa Tanzania wanaitwa wanyonge) na kuwapandisha kwenye hali nzuri.

Baadhi ya Wakenya wakamuamini na kuachana na Raila Odinga, ambaye alikuwa na nafasi kubwa ya ushindi kabla ya kutafunwa na laana kutokana na kuunga mkono udikteta wa serikali ya kikatili ya Tanzania iliyoongozwa na John Magufuli.

Cha kushangaza sasa baada ya Rutto kupata urais, akasahau haraka sana mkakati wake kwenye Bottom Up mithili ya mtu aliyelogwa ili asahau kwao, akaanza kuondoa ruzuku zilizowekwa na watangulizi wake ili kudhibiti bei ya mafuta, akidai anabana matumizi, utadhani hela za Kenya ni mali ya baba yake, bei ya mafuta ikainuka na hatimaye ikainua na bei za vitu vingine na kusababisha ugumu wa maisha ambao haukuwahi kuwepo tangu Yesu alipoondoka Galilaya.

Sasa Wakenya wamekiwasha mitaani wanataka kumng'oa.

Mungu ibariki Jamhuri ya Watu wa Kenya.
Kusema kuwa una falsafa za bottom up na kuondoa ruzuku haimaanishi kwamba ni automatic contradiction.

Hususan ikiwa ruzuku hazikuwa na tija na hela hizo zinaweza kutumika kwa tija zaidi katika uchumi na hatimaye kunufaisha uchumi mzima.

Simtetei Ruto wala kutoa maoni yoyote kwenye siasa za Kenya zaidi ya kusema kwamba kusema Rais kasahau bottom up, kwa sababu kaondoa ruzuku, ni a very simplistic way of thinking.
 
Bottom up ni nini na utekelezaji wake ni upi na utaanza lini ?
 
Back
Top Bottom