SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wengi wanaamini upigaji penati ni bahati zaidi ya ufundi ila mimi napingana na hiyo dhana. Nikiwa mtu niliyecheza mchezo huu wa football kwa kiwango kikubwa sana katika nafasi tofauti uwanjani na kuna wakati nikawa hadi kocha, nina uwezo wa kulizungumza hili kwa uhakika na kujiamini maana najua ninachozungumza.
Kuna vitu fulani vidogo tu ambavyo mpigaji penati ukivijua, kukosa penati itakuwa ni nadra sana. Vivyo hivyo ukiwa golikipa kuna vitu ukivifahamu chance ya kuzuia penati inaongezeka maradufu na vyote hivi vinahusiana na saikolojia.
Nimemshuhudia golikipa Yassine Bounou, maarufu kama Bono, mchezaji wa Sevilla na timu ya taifa ya Morocco kama mmoja wa magolikipa waliomasta saikolojia ya kudaka penati.
Bono niliona umahiri wake katika Kombe la Dunia la 2022 kule Qatar. Nilimuangalia kwa makini sana vitu alivyokuwa anavifanya wakati wa penati na ni vitu ambavyo siku zote naamini ndiyo mbinu za kudaka penati.
Katika picha hii hapa juu, Bono alidaka penati hii huku anacheka baada ya kumuhadaa mpigaji naye akaingia mazima.
Jana katika mechi ya fainali ya kombe la EUROPA kati ya AS Roma na Sevilla, nilimuona tena akifanya vitu hivyo hivyo na akaokoa penati 2 zilizoipa ubingwa Sevilla.
Kwenye upigaji au kudaka penati, trick ipo kwenye kupenya kwenye kichwa cha mchezaji wa upande wa pili na kucheza na akili yake ili kumuhadaa akili yake. Ni kitendo cha sekunde chache sana ila ukikipatia matokeo yake utayaona. Ukifanya hivi, utajua usimame vipi na ucheze vipi na mikono na mwili wako kiujumla.
Kama unataka kujua mbinu za udakaji penati, msome vizuri golikipa wa Sevilla na timu ya taifa ya Morocco, Bounou.