Huwa sielewi mimi ndio mjinga au sielewi akili za watu wa mpira. Jamaa kadai ni fani yake ila anavyoeleza utadhani kasimuliwa leoleo yani kama kaokoteleza maelezo kidogo.
Huwezi ona mtu anajiita fundi mzoefu wa magari simply anakwambia "fanya service". Atakwambia mwaga oil, tumia oil husika, usifanye hiki, kama kuna tatizo fulani fanya hivi.
Kucheka kwa Bono kulimfanyaje adake penati?
"Kwenye upigaji au kudaka penati, trick ipo kwenye kupenya kwenye kichwa cha mchezaji wa upande wa pili na kucheza na akili yake ili kumuhadaa akili yake..."
ndio nini hapa? Mpigaji au kipa anapenyaje kwenye kichwa cha mwenzake, tricks zipi anatumia, sign zipi anaona.
Wewe ni kocha ila umeandika kama nabii, hana haja ya kujua sana atawasingizia waumini wawe na imani basi hata kama hamna logic