Hafu Thunderbolt wanakuja soon, unawajua thunderbolt??[/QUOTE]
Hawa jamaa niliwasoma kwenye comics
Story yao iko hivi
Baada ya vita na yule mutant adui Onslaught kuondoka ulimwenguni bila mashujaa wengi ambao waliifanya iwe salama, nasemea avengers Baron Zemo alipanga mpango ili kutawala ulimwengu.
Zemo alikusanya kikundi chake kina Beetle, Fixer, Goliath, Moonstone, na Screaming Mimi, wote washiriki wa zamani wa Masters of Evil, yaani wote walikuwa villan pamoja kujificha kama timu mpya ya kishujaa ili kuchukua faida ya mashujaa waliopotea na kupata imani kwa mamlaka na umma kwa ujumla.
Yaani walifanya kama vile Ile season ya the boys wanajifanya super heroes kina homelander sjui outlander sikumbuki vzr jina yule jamaa maana niliichek kitambo season 1 episode chache tu .basi bhana kumbe wana motive zao ni maadui
Hivyo basi walijiunga na jamaa mdogo tu ambae alikuwa anapenda awe celebrity awe star anaitwa Jolt, ila yeye hakujua utambulisho wa kweli wa wenzake na ajenda iliyofichwa.
Zemo alikuwa hampendi Jolt na anamvumilia kwenye hicho kikundi chake lakini wenzake walimpenda haraka na kuanza kubadilishwa na maoni yake
Ila baadae sasa
Zemo ghafla aliacha udanganyifu wao akazindua mpango wa kuchukua ulimwengu kwa kuwatumikisha kila mtu pamoja na Avengers wanaorudi maana walitawanyika pamoja na wale heroes fantastic four
HApa sasa utaona kama hii comics wameifanya iwe movie.basi jua tutapata kuwaona avengers kwa mara nyingine tena si ajabu next avengers movie avengers reassemble
Halafu sasa [emoji28] cha ajabu marvel walivyo introduce fantastic four nikasema ewaaa hawa jamaa washa confirm theory yangu
Maana huwezi kuwa introduce thunderbolt bila fantastic four na avengers kuwepo wanatengeneza story ya aina yake kama vile infinity saga maana tutakuja kuwa na cameo appearance huko mbeleni za kufa mtu
Lakini kwenye comics tunaona na wale washiriki wa zemo waliamua wanapendelea maisha ya ushujaa kuliko mwovu maana walifungua mioyo yao vile kusaidia watu na wakaungana na Iron Man kumaliza mipango ya Zemo.
Mwishowe, Zemo alikimbia na washirika wake waliofata msimamo wake ili kuanza maisha mapya kwa kukimbia kama washambuliaji haramu, wakijaribu kudhibitisha ushujaa wao kwa umma wakati wakikwepa kukamatwa.
So conclusion hapa thunderbolt Ni villain ambao.baadae wanakuwa hero.
Tukiangalia kwenye movies.kwenye marvel cinematic universe na maoni mengi ya watu plus spoilers
Tunaona yule zemo wa Falcon na winter soldier anaweza kuwepo ndo maana kipande chake akiwa jela kumeonyeshwa last episode
HApa kuna yule incredible hulk anaweza wepo yaani haijajulikana.
Na character wengine wapya