Boxing: Anthony Joshua apigwa na kuvuliwa mikanda yake na Andy Ruiz Jr

Mexician rock ameonyesha ukakamavu na kumuonyesha yule mwehu Big baby miller boxing sio maneno maneno..

AJ alikuwa anavuta muda na zile jab jab amalize na right akiamini mexician rock atachoka amaliza pambano akasahau jamaa ana good punches na speed at the end AJ went down looking too tired and fatigue..
 
Kwani pambano lake na miller baby imekuwa vipi

Big baby Miller fala yule, alipimwa drugs kitu kikasoma positive akanyimwe leseni, ikabidi atafutwe mbadala maana pambano liliandaliwa toka january ndio akapatikana "Mexician rock" Andy Luis Jr.

Naamini Big baby kwa AJ asingefikisha hata round ya tano, maneno mengi sana fala yule..
 
#KWA UFUPI: Bondia, Andy Ruiz Jr ameweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza wa Mexico kushinda pambano kubwa la ngumi duniani baada ya kumtwanga bingwa wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua kwa TKO katika raundi ya 7. Mpambano uliofanyika New York Marekani alfajiri ya leo.

Source: https://www.google.com/amp/s/www.bbc.com/swahili/amp/habari-48487906

------
Andy Ruiz Junior sasa ndio bingwa mpya wa ndondi duniani baada ya kumrambisha sakafu Anthony Joshua

02 Juni 2019

Sambaza habari hii Email Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Whatsapp

Image copyrightGETTY IMAGES[https://ichef-bbci-co-uk]

Bondia wa uzani mzito ameushangazwa ulimnwengu ka kumshinda bingwa wa ndondi katikja uzani huo Anthony Joshua

Joshua ambaye amepigiwa upatu kumrithi bingwa wa zamani katika uzani huo Mohamed Ali aliangiushwa mara nne kabla ya refa kuingilia kati na kusitisha pigano hilo kunako raudni ya tatu.

Andy Ruiz Jr aliushangaza ulimwengu katika historia ya ndondi na kufanikiwa kushinda mataji ya IBF, WBO na WBA yaliokuwa yakimilikwa na Anthony Joshua.

Katika pigano lililovutia wengi katika ukumbi maarufu wa ndondi nchini Marekani Mew York Madison Square Garden , Ruiz alimuangusha Joshua mara nne kabla ya kumuangusha katika raundi ya saba hatuailioushangaza ulimwengu.

Joshua alipigiwa upatu kushinda pigano hilo na wengi kwa urahisi huku wachanganuzi wakifananisha pigano hilo na lile la Lennox Lewis na Mike Tyson kama mabondia walioshindwa na kusababisha hali ya sitofahamu katika ndondi duniani.

Sio Joshua anayejulikana na Uingereza

Na haikuwa bahati mbaya kwa Joshua kwani alikuwa amepigwa kutoka raundi za kwanza alipomuangusha Ruiz.

Na baada ya kupigwa ngumi kali ya kushoto , Joshua aliangukia kamba za ukumbi wa ndondi .

Na kabla ya kukamilika kwa dakika tatu za raundi hiyo aliangushwa tena bada ya Ruiz kumshambulia kwa mchanganyiko wa makonde .

Hatua hiyo iliwashangaza wengi katika ukumbi wa Madison Square Garden,

Image copyrightGETTY IMAGES[https://ichef-bbci-co-uk]

Hatua hiyo iliwashangaza wengi katika ukumbi wa Madison Square Garden,

Je ni nini kilichotokea?

Image copyrightREUTERS[https://ichef-bbci-co-uk]

Ruiz ambaye alishirikishwa katika pigano hilo baada ya raia wa Marekani Jarell Miller kupatikana na dawa za kusisimua misuli wiki sita tu kabla ya pigano hilo.

Na ilipofikia raundi ya saba , wakati Joshua alipoangushwa mechi hiyo ilikuwa imekwisha baada ya kupigwa ngumi nyingi zilizomchanganya na kulazimika kutema kifaa kinacholinda meno.

Hakuwa nacho mdomoni na refa alipoona Joshua kachanganyikiwa aliingilia kati na kusitisha pigano.

Ruiz alionekana hafifu sana kuweza kumshinda bingwa huyo wa ndondi sio tu kwa maneno bali hata kwa maungo.

Waingereza watakapoamka siku ya Jumapili alfajiri watashangazwa na matokeo haya.

Pigano la marudio kabla ya mwisho wa mwaka

Joshua alikuwa ameshindwa katika raundi pili akishinda moja wakati alipopigwa knockout lakini atapata fursa ya kujirekebisha katika mechi ya marudio jijini London , kabla ya mwezi Disemba kulingana na promota Eddie Hearn.

Kwa sasa mazungumzo yoyote ya kuzipiga dhidi ya Tyson Furry ama hata Deontay Wilder yamesitishwa.

Ruiz ambaye kwa sasa ameshinda mara 33 na kupoteza mara moja aliruka ruka katika ukumbi wa ndondi wa Madison Square Graden baada ya refa kusitisha pigano hilo.

Anajiunga na James Buster Douglas ambaye alimshangaza Tyson na Hasim Rahman ambaye alimpiga Lewis mwaka 2001 kama mmojawapo wa mabondia walioushangaza ulimwengu. Lewis alijibu kwa kushinda pigano la marudio.

Ruiz hatahivyo alionyesha uwezo mkubwa katika pigano hilo ikimaanisha kwamba Joshua atakuwa na kazi ya ziada kumshinda katika pigano hilo linalotarajiwa kufanyika kabla ya mwaka kukamilika mjini London.
 
Joshua ana maneno mengi sana. Bora wamemnyamazisha.
 
Mexician Rock ni mfupi lakini he has the good punches and speed except his bad body compared to AJ.. AJ alikuwa anajaribu Lenox Lewis style ili amshoshe Mexician rock lakini inaonekana ile jab yake haina nguvu kama ya Lewis ilivyomchosha tyson..

All in All was a classic fight from Mexician rock because he came as the underdog to AJ but shows its possible for the fat to win over the fit.. Short man with good punches and fast combinations shows the world he is classical and can be the future white Mike Tyson...
 
Aisee AJ kakalishwa down!!!

[emoji15][emoji15]
 
Nimekosa kuona hili pambno, itanibidi nitazame highlights
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…