Kingkorlar
JF-Expert Member
- Oct 16, 2018
- 875
- 995
Hata akitaka Rematch wanampiga tena
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata akitaka Rematch wanampiga tena
Hii ndy kauli ya kimichezoNiliacha Kufuatilia Mchezo wa Masumbwi hasa ile miaka ya akina Tyson na Evander ila hapa Juzi kati nilipokuwa nikitizama sana TV1 na Kuangalia Mapambano ya huyu Bondia Antony Joshua kiukweli hata kama Jana amepigwa huko ila amenifanya nianze tena kuwa Shabiki wa Mchezo wa Masumbwi kwani Antony Joshua ni Bondia mzuri sana na ameiga vyema mno nyayo za Mike Tyson na Lenox Lewis, ana ' Endurance ' ya hali ya juu, Mjanja awapo Ulingoni ila Kikubwa zaidi anachonivutia nacho Antony Joshua ni kwamba ana Nidhamu ya hali ya juu, hana Maringo na ana ' Spirit of Sportsmanship ' ya ukweli kabisa. Nampongeza pia na huyo Bondia Ruiz kwa Kushinda na nadhani huu utakuwa ni mwanzo mwema / mzuri Kwake na Yeye sasa kuwa ' Mbabe ' wa dunia baada ya Joshua ' Kutawala ' kwa Kipindi kirefu.
Hatimaye yule mbabe wa masumbwi ya Uzito wa juu duniani Anthony Joshua kutoka nchini Uingereza,usiku wa jana kuamkia leo amepokea kipigo kikali kutoka kwa Bondia mwenye umbo kama "kitimoto" Mmexico Andy Ruiz mwenye makazi yake California, nchini Marekani. Pambano hilo lilipigwa katika ukumbi wa Madison Square Garden, Newyork. Joshua alionyesha uhai kidooogo katika raundi ya tatu alipomuangusha mpinzani wake kwa konde zito,naye Ruiz alijibu mapigo kwa nguvu zote na kumlambisha sakafu mara mbili Anthony Joshua katika raundi hiyo ya tatu.Kiukweli AJ hakuwaweza kuonyesha makali yake kama tunavyomfahamu,yaani alikuwa anapigana kama hataki hali iliyopelekea mpinzani wake kumsukumia makonde mengi ya uso.Raundi ya 7 ndio ilikuwa mbaya sana kwa AJ alilambishwa sakafu mara mbili tena na kwenda angle yake, ambapo mwamuzi alimuuliza kama yuko tayari kuendelea lakini alikataa na kuwa mwisho wa game. Nilikuwa nampa AJ 100% za ushindi lakini imekuwa kinyume na matarajio yangu. Pambano hili limenikumbusha pigano la mwaka 1990 kule Tokyo nchini Japan kati ya Mike "Iron" Tyson na James Douglas "Buster" hakika kwa wale wakongwe waliokuwa wakimfuatilia Tyson kwa kila pambano alilokuwa akicheza hawakuamini kilichotokea huko Japan,kiukweli Tyson alikuwa na mashabiki wengi sana duniani kwa hiyo alipopigwa na James Douglas wengi hawakuamini walibaki na simanzi na baadhi walitokwa machozi kwa Tyson kushindwa. Ndicho kilichomtokea AJ ambaye usiku wa jana kuamkia leo. Mara nyingi tumeona kila mchezo anaocheza AJ anashinda. Hatimaye historia ya 1990 imejirudia. Kwa hiyo AJ amepokonywa mikanda yote mitatu aliyokuwa anaihold.
Uzuri wa Andy sio defensive player, ni attacking destroyer na anajua kukwepa, kilichompoteza AJ kila akipiga jamaa analipa more times, afu alimu underrate Andy, lakini Andy alimuonya mapema kuwa unanichukulia poa ngoja nitakufundisha nidhamu. Sipendi mabondia wanaopambwa kwa kuchagua wapinzani dhaifu.
Naamini lazima AJ aombe rematch na Andy Jr before the end of this year . itakuwa mechi yenye Pesa ndefu though haitofikia km wakikutanishwa na Wilder a.k.a bomber