Boxing: Anthony Joshua kupanda ulingoni tarehe 28/10/2017 kupambana na Kubrat Pulev

Boxing: Anthony Joshua kupanda ulingoni tarehe 28/10/2017 kupambana na Kubrat Pulev

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Bondia machachali asiyekuwa na maneno mengi bali vitendo anapokuwa ulingoni AnthonyJoshua (28)hatimaye ametangaza kuwa atapanda ulingoni mnamo tarehe 28 October 2017 kutetea mikanda yake ya WBF,IBO na IBF dhidi ya Kubrat Pulev(36) katika uwanja wa Millennium Stadium (Cardiff Prinvipallity Stadium)

AJ ambaye mwezi April mwaka huu alipanda ulingoni na kuzichapa na mkongwe Vladimir Klitchko na kufanikiwa kumtwanga kwa Knockout amepambana jumla ya mapambano 19 na yote ameshinda kwa K.O.

Kubrat Pulev ana rekodi ya kupambana mapambano 26 na kushinda mapambano 25 huku akipoteza pambano moja.

13 kati ya hayo 25 Pulev ameshinda kwa K.O.

Mashabiki wengi wa mchezo wa boxing duniani wamekuwa na mtazamo wa tofauti kuhusu mpambano huu ingawaje asilimia kubwa wamempa AJ kushinda kwa K.O licha ya uwezo mkubwa alionao Pulev.

Pambano ambalo mashabiki wengi walitarajia kuliona ni kati ya AJ na Deontay Wilder(Bronze Bomber)wakiamini ndiye mtu sahihi zaidi wa kupambana na AJ.

Screenshot_2017-09-05-20-25-48.jpg



Screenshot_2017-09-05-20-25-34.jpg
 
Hizi hilo jambazi mywether akijichanganya si linaua kabisa
 
Boxing is a barbaric game.

Karume was right.
 
Back
Top Bottom