Boxing | Arturo Gatti v Micky Ward: Pambano bora la muda wote

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Hii dunia imeshuhudia mabondia wengi mahiri na wenye uwezo mzuri wanapokuwa kwenye ring.

Tumeshuhudia mabondia kama Tyson, Holyfield, Lennox Lewis, na kona Forman kwenye uzito wa juu.

Kina Ray jones na wenzie kwenye uzito wa juu kati. Kisha uzito wa kati kina mywether jr, Pac, Canelo na kina GGG.

Nimeangalia pambano kati ya Khan na maidana, Canelo na GGG, mywether na pacman. Matthyesse na Ruslan. Mapambano yalikuwa moto.

Lakini kati ya pambano bora kwangu ni pambano la uzito wa kati, kati ya Arturo Gatti na Micky Ward. Hawa jamaa wamepigana mara tatu. Ward akishinda moja, Gatti akishinda moja na kutoa sare 1.

Huu mpambano wao ni balaa. Jamaa walipigana ngumi zisizo na idadi. Kila round ni moto.

Kwako pambano bora kabisa ni lipi?

 
Wewe kweli wajua boxing.
Mimi pambano langu Kali litakua la AJ na Wilder. Likijakutokea. Sio kwamba sina mengine ila natamani hilo
 
NI HIVII:-

Kama kweli unafuatilia WBC hasa ''Heavy weight'

Kuna mapambano makali ya mabondia wakali wa muda wote....!

-Muhammad Ali VS George Foreman, ''The RUMBLE IN THE JUNGLE'' waliopigana 29 / 10 / 1974 Kinshasa - Zaire ya wakati huo na Congo la leo.

-Muhammad Ali VS Joe Frazier - Hawa walipigana Mara 3

-George Foreman VS Frazier

-Lennox Lewis VS Vitali Klitschko

-Holyfield Evander VS Lennox Lewis

-Mike Tyson VS Holyfield Evander

-Mike Tyson VS Bruno

KWISHA...!

Baada ya hapo kwakweli Boxing imepoteza mengi na imekuwa kibiashara zaidi. Kina Anthony Joshua wasasa ni Heavy weight ambao hawana la maana kwakweli.

Kama Evander angepigana na hawa wa leo angeshinda kila siku.
 
Ebwana pambano LA canelo na GGG cjawah kuona aisee wajomba wanapigana makonde halaf wamesimama tu yaan mwanzo mwisho. Hilo Ndó pambano langu kali kuliko yote. Na natumain watarudiana tena kwa Mara ya 3.

Ila GGG juzkat nmechek pambano Lake LA mwisho jamaa alishinda Kwa kubebwa kabisa akirudiana na canelo sijui itakuwaje
 
Upo sawa. Kuna tofauti kati ya pambano bora na pambano kubwa. Hayo uliyotaja hapo ni mapambano makubwa. sawa na lile la Man paq na Floyd Maywether. Hili pambano lilipewa jina Fight of century lakini tulichoona ni tofauti na wengi tulichtarajia.

Kina fraizer, Forman walikuwa wakali, na walikuwa wakilinganishwa na mkali wao wa wakati huo Muhamed Ally.

Ila Gutti vs Ward ni habari ingine. Pambano lao baada ya kupigana likapewa jina fight of decade.

Nashukuru Mods wamenisaidia kuattach video.
 
Moja kati ya mtihani mgumu kwa Canelo aliowahi kupambana nao. Caneno amepoteza pambano 1 tu tena dhidi ya bondia bora wa wakati waote. Floyd Maywether jr. Tena Canelo akiwa dogo kabisa. Ilikuwa 2013 nadhani ndio kwanza alikuwa na 23 yrs kama sikosei.

GGG nae ni moto mkali.
 
Ilisemwa kuwa uzito wa ngumi zilizorushwa kwenye hili pambano unatosha kuangusha hata gorofa
rope -a -dope, hili ndilo pambano bora kabisa la ngumi kuwahi kutokea hapa dunia kati ya Muhammad Ally Vs George Foreman mwaka 1974 pale Manila, Ufilipino.
 
Rumble in the Jungle
Pambano lilifanyika pale Kinshasa, Zaire kwa Mobutu Sesseseko Kukubendu Wazabanga
 
zama za Kina Muhammed Aly sie wengne bado hatukuwa duniani. Ila tulibahatika kuwashuhudia mabondia wa kwl AkinaMyke Tyson, Evander Holyfield, Lennon Lewis, Bruno na wengine.. hawa mabwana kwl walikuwa wanapiga makonde si mchezo.
Ila mabondia hawa wa kileo kuanzia Uzito wa juu akina Anthony Joshuo mpk uzito wa kati akina Floyd Myweather, Pac Man Paquiao hamna kitu.. ni mbwembwe nying na kibiashara zaid
 
James William vs Tyson nihatarii sana mwaka 2004
 
Fight of the century
Fraizer vs alli..... Alli akipoteza kwa mara ya kwanza

Floyd vs canelo.... Mayweather niliipenda style yake ya defensive huku akidokoa kama pakaaa....
 
Fight of the century
Fraizer vs alli..... Alli akipoteza kwa mara ya kwanza

Floyd vs canelo.... Mayweather niliipenda style yake ya defensive huku akidokoa kama pakaaa....
Ulibahatika kuona mpambano wa Lucas Matthyesse na Ruslan au Maidana na Khan.

Watu ni sugu jamani! Ruslan alipata kipigo cha mbwa koko, ila alimtoa jasho Matthysse.

Ngumi zinarushwa balaa.

Unawazungumziaje wakali wa sasa. Errol spencer jr, Gevronta Davis Tank na Crawford?
 
Maugo alifika round ya 7 akatoka uwanjani...akasema hamuoni mpinzani wake anapigana na hewa,anajikuta anapigwa tu hajui anaemshambulia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mada maugo vs cheka mzee wa miziziology

Hawa jamaa walikua wakipigana ni burudani sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…