Boxing | Arturo Gatti v Micky Ward: Pambano bora la muda wote

Mkuu hiyo ya Ruslan sikufanikiwa kuuona...
Ila weka mbali kabisa huo mpambano wa el chino vs khan the king himself hii pambano ilikua hatari sana.. Nilidhani inaweza kuisha round ya kwanza baada ya maidana marcos el chino kupokea left hook nzito iliyomplka chini...daah sema mwamba aliugulia maumivu akaamka tenaa... Ile pambano ilikua nikali na nafikiri maidana Ali deserve ushindi sema fitna tuuh hakupewa coz khan kila saa alikua anabanwa kwenye angle na kupelekewa uppercut za kutosha sjui kilitokea nn jamanii...
Ulibahatika kuona mpambano wa Lucas Matthyesse na Ruslan au Maidana na Khan.

Watu ni sugu jamani! Ruslan alipata kipigo cha mbwa koko, ila alimtoa jasho Matthysse.

Ngumi zinarushwa balaa.

Unawazungumziaje wakali wa sasa. Errol spencer jr, Gevronta Davis Tank na Crawford?
 
Ulicheki battle of the titans...
kati ya (the lion na dr. iron fist).... Hii ndo kali yangu ya miakaa yotee sababu lennox alisababisha nione sisi mablack ni powerfully kwa body power...
Hii dunia imeshuhudia mabondia wengi mahiri na wenye uwezo mzuri wanapokuwa kwenye ring.

Tumeshuhudia mabondia kama Tyson, Holyfield, Lennox Lewis, na kona Forman kwenye uzito wa juu.

Kina Ray jones na wenzie kwenye uzito wa juu kati. Kisha uzito wa kati kina mywether jr, Pac, Canelo na kina GGG.

Nimeangalia pambano kati ya Khan na maidana, Canelo na GGG, mywether na pacman. Matthyesse na Ruslan. Mapambano yalikuwa moto.

Lakini kati ya pambano bora kwangu ni pambano la uzito wa kati, kati ya Arturo Gatti na Micky Ward. Hawa jamaa wamepigana mara tatu. Ward akishinda moja, Gatti akishinda moja na kutoa sare 1.

Huu mpambano wao ni balaa. Jamaa walipigana ngumi zisizo na idadi. Kila round ni moto.

Kwako pambano bora kabisa ni lipi?

Mkuu hiyo ya Ruslan sikufanikiwa kuuona...
Ila weka mbali kabisa huo mpambano wa el chino vs khan the king himself hii pambano ilikua hatari sana.. Nilidhani inaweza kuisha round ya kwanza baada ya maidana marcos el chino kupokea left hook nzito iliyomplka chini...daah sema mwamba aliugulia maumivu akaamka tenaa... Ile pambano ilikua nikali na nafikiri maidana Ali deserve ushindi sema fitna tuuh hakupewa coz khan kila saa alikua anabanwa kwenye angle na kupelekewa uppercut za kutosha sjui kilitokea nn jamanii...
Hahahahahah Maidana alikuja kuonekana kuanzia round ya tano kama sikosei. Round zote za mwanzo alipokea kipigo cha maana toka kwa khan.khan anarusha jeb za fasta na kumkimbia.

Round ya 9 kama sio ya kumi, Maidana anamjaza ngumi nzito khan anapoteza mwelekeo. Kengele inamwokoa khani. Round ya 11 na 12 maidana anashinda zote.

Ila kwa ujumla kwa maoni yangu Khani alistahili huo ushindi.
 
Pambano langu bora kabisa la muda wote ni kati ya Mike Tyson na Jesse Ferguson la Mwaka 1986 ililofanyika NewYork, bonge la pambano ngumi zilipigwa balaa mwishowe Ferguson akasalimu amri raundi ya sita.
 
Canelo Vs GGG, mapambano yote mawili ni moto wa kuotea mbali, mikono inapigwa mule si mchezo
 
Pambano langu bora kabisa la muda wote ni kati ya Mike Tyson na Jesse Ferguson la Mwaka 1986 ililofanyika NewYork, bonge la pambano ngumi zilipigwa balaa mwishowe Ferguson akasalimu amri raundi ya sita.
Lile ambalo wanakumbatiana kila sekunde? Kiukweli ukitaka kuangalia mapambano ya ukweli ambayo mikono inapigwa na unapata burudani, no kushikana angalia mapambano ya uzito wa chini
 
Pambano langu bora kabisa la muda wote ni kati ya Mike Tyson na Jesse Ferguson la Mwaka 1986 ililofanyika NewYork, bonge la pambano ngumi zilipigwa balaa mwishowe Ferguson akasalimu amri raundi ya sita.

Kwani huyo Jesse Ferguson alifanya nini cha maana cha kukumbukwa ktk mpambano huo?
Mimi nakumbuka kama vile niliona vumbi tu toka kwa Jesse.
 
Thrilla in Manila, lilipigwa pambano ambalo ni kama ilikuwa mwisho wa dunia kwa mabondia wale. Yalirushwa makonde na ngumu za aina yake! Bado linabaki pambano bora kwa upande wangu
 
MIKE TYSON NA BRUNO FRANK? 😳😳😳😳😳 Hamna kitu pale kabisa.
NI HIVII:-

Kama kweli unafuatilia WBC hasa ''Heavy weight'

Kuna mapambano makali ya mabondia wakali wa muda wote....!

-Muhammad Ali VS George Foreman, ''The RUMBLE IN THE JUNGLE'' waliopigana 29 / 10 / 1974 Kinshasa - Zaire ya wakati huo na Congo la leo.

-Muhammad Ali VS Joe Frazier - Hawa walipigana Mara 3

-George Foreman VS Frazier

-Lennox Lewis VS Vitali Klitschko

-Holyfield Evander VS Lennox Lewis

-Mike Tyson VS Holyfield Evander

-Mike Tyson VS Bruno

KWISHA...!

Baada ya hapo kwakweli Boxing imepoteza mengi na imekuwa kibiashara zaidi. Kina Anthony Joshua wasasa ni Heavy weight ambao hawana la maana kwakweli.

Kama Evander angepigana na hawa wa leo angeshinda kila siku.
 
Ulibahatika kuona mpambano wa Lucas Matthyesse na Ruslan au Maidana na Khan.

Watu ni sugu jamani! Ruslan alipata kipigo cha mbwa koko, ila alimtoa jasho Matthysse.

Ngumi zinarushwa balaa.

Unawazungumziaje wakali wa sasa. Errol spencer jr, Gevronta Davis Tank na Crawford?
Mkuu nimecheki Hilo pambano laatthyesse ve ruslan ni hatari ...

Haya mapambano mengine ni majina tu
 
Rashid matumla vs Joseph Marwa
. Only legends will get me!
 
Hii dunia imeshuhudia mabondia wengi mahiri na wenye uwezo mzuri wanapokuwa kwenye ring.

Tumeshuhudia mabondia kama Tyson, Holyfield, Lennox Lewis, na kona Forman kwenye uzito wa juu.

Kina Ray jones na wenzie kwenye uzito wa juu kati. Kisha uzito wa kati kina mywether jr, Pac, Canelo na kina GGG.

Nimeangalia pambano kati ya Khan na maidana, Canelo na GGG, mywether na pacman. Matthyesse na Ruslan. Mapambano yalikuwa moto.

Lakini kati ya pambano bora kwangu ni pambano la uzito wa kati, kati ya Arturo Gatti na Micky Ward. Hawa jamaa wamepigana mara tatu. Ward akishinda moja, Gatti akishinda moja na kutoa sare 1.

Huu mpambano wao ni balaa. Jamaa walipigana ngumi zisizo na idadi. Kila round ni moto.

Kwako pambano bora kabisa ni lipi?

Kwel Mkuu hili pambano ni hatari . R i p gatti
 
NI HIVII:-

Kama kweli unafuatilia WBC hasa ''Heavy weight'

Kuna mapambano makali ya mabondia wakali wa muda wote....!

-Muhammad Ali VS George Foreman, ''The RUMBLE IN THE JUNGLE'' waliopigana 29 / 10 / 1974 Kinshasa - Zaire ya wakati huo na Congo la leo.

-Muhammad Ali VS Joe Frazier - Hawa walipigana Mara 3

-George Foreman VS Frazier

-Lennox Lewis VS Vitali Klitschko

-Holyfield Evander VS Lennox Lewis

-Mike Tyson VS Holyfield Evander

-Mike Tyson VS Bruno

KWISHA...!

Baada ya hapo kwakweli Boxing imepoteza mengi na imekuwa kibiashara zaidi. Kina Anthony Joshua wasasa ni Heavy weight ambao hawana la maana kwakweli.

Kama Evander angepigana na hawa wa leo angeshinda kila siku.
Mkuu Vip kuhusu Riddik bowe vs Evander
 
Mkuu Vip kuhusu Riddik bowe vs Evander
Bowe vs Holyfied ,was one of the best feuds in boxing . Japo nilitamani sana kuona nani mbabe kati ya Lenox na Bowe , waliwahi kuzichapa wakiwa wadogo kweny olimpic games.
 
Kwel Mkuu huo mpambano ungekuwa wa hatari.
 
Back
Top Bottom