BP na nguvu za kiume

duocore

Member
Joined
Aug 27, 2012
Posts
55
Reaction score
5
Wana JF naomba mnijuze, je bp inaweza punguza nguvu za kiume? matumizi dawa za kudhibiti bp nazo zaweza sababisha nguvu za kiume? na je, ni ipi tiba nzuri ya bp ya asili? asanteni.
 
Mambo yanayochangia Upungufu wa nguvu za kiume

LEO ninataka tuangalie kwa kina mambo yanayochangia tatizo hilo upungufu wa nguvu za kiume.

Ningependa tulio katika ndoa, ukishaisoma makala hii tuwahusisishe wenza wetu nyumbani au mpigie rafiki yako na kumueleza kuwa ana nafasi ya kujilinda kupoteza nguvu za kiume na hivyo kuwa na uhakika wa amani nyumbani.

Nasema amani kwa sababu tatizo hili huingilia amani nyumbani kwani kuna kuhisiwa kuwa mwanaume anajihusisha na nyumba ndogo maarufu. Uzoefu katika vituo vyetu vya Marie Stopes kina mama ndio huja kutafuta ushauri kwa nini mzee kabadilika na wafanye nini ili kumrudisha nyumbani. Zifuatazo ni sababu amabazo kitaalamu zinatajwa kuchangia kupungua kwa nguvu za kiume na nyingi kama si zote zinaepukika.

Msongo wa mawazo: Ni dhahiri kuwa akili na tendo la ngono vinategemeana sana. Inajitokeza mara nyingi sana kwa watu wenye matatizo katika biashara, kazini na sehemu nyingine hujikuta hawako katika hali ya kuwa na hamu ya tendo la ndoa mpaka pale watakapotulia. Hii inaweza kuwapata watu wa rika zote na tatizo hili linaweza kuisha haraka kutegemeana na shughuli zao zinavyorudi katika hali ya kawaida.

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
Mzunguko wa damu mwilini una maana sana kwani kama damu haizunguki vizuri itachangia uume kutosimama vizuri kwa sababu usimamaji hutegemea kiasi na kasi ya damu inayoingia kwenye mishipa ya sehemu hiyo. Dawa zinazotumika kutibu shinikizo la damu huchangia pia kupungua kwa nguvu za kiume.

1. Unywaji pombe kupita kiasi: Pombe inaweza kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu kwa wakati mmoja. Wakati mwingine mtu akilewa sana huathiri ubongo na kukata mawasiliano kisaikologia na hivyo kushindwa kuwa katika hali ya kuwa na hamu ya ngono na hivyo kutosimamisha.

2. Unene. Unene huwa unaambatana na mafuta mengi mwilini. Mafuta hayo wakati mwengine huzidi kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu na hivyo kupunguza ukubwa wa mrija kiasi kwamba damu inipita kidogo na kwa shida. Hii huchangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa sababu kiasi cha damu kinachotakiwa kisimamisha uume kitakuwa kidogo sana. Wakati mwingi uume unaweza kusimama kidogo na kulala kabla shughuli haijakamilika.

3. Kutokufanya mazoezi: Tusipofanya mazoiezi pia mzonguko wa damu kutokuwa mzuri na hivyo kutoparuhusu damu ya kutosha kusimamisha uume. Kwa watu wanaotembelea magari na shughuli za kukuaa maofisini mda mrefu na hasa kama hawafanyi mazoezi asubuhi au jioni wako kwenye hatari zaidi kuliko watu wanotembea kwa miguu mwendo mrefu na kufanya kazi ngumu za kuuchosha mwili.

5. Matatizo ya kisukari: Kisukari ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kufanya mishipa ya damu kutofanya kazi yake viuri ili kuruhusu damu kujaa kwenye uume. Hii himfanya mgonjwa wa kisukari kushindwa kusimamisha hata kama ana hamu ya kufaya tendo hilo.

5. Umri:
Inaelezwa kuwa kadri umri unavyopanda ndio uwezo wa nguvu za kiume utaendelea kupungua. Baadhi ya watu huanza kuona tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40 na kuendelea na hasa kama maisha yao hayakuwa na mazoezi ya mwili.

Sababu nyingine ni kama utumiaji madawa ya kulevya, kuumia katika uti wa mgogongo, uvutaji sigara nk. Sababu nyingi zinachangia kupungua kwa nguvu za kiume zinaepukika kwa hiyo tunashauriwa kuwasiliana na wataalamu ili kujifunza jinsi ya kujikinga au kutibu matatizo hayo.

https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/196934-dawa-za-nguvu-za-kiume-kwa-anayetaka.html
 
Ni kweli Bp inaweza kukuletea upungufu wa nguvu za kiume hasa isipotibiwa. Lakini kunadawa za Bp kama Beta blockers husababisha upungufu wa nguvu za kiume hivyo mara nyingi huwa hatuwapi vijana au wagonjwa waliokwenye umri wa kuzaliana. Mfano wa dawa hizo ni kama Atenalol, propranalol n.k.
Pole mkuu jitahidi kuzingatia vyakula na mazoezi matatizo haya hupungua. Kazi njema
 
Doctor wa kweli Mupirocin,

Umenena. duocore zingatia hayo!!


Mudushi

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…