Hakuna mwenye akili unayoifikiria wewe kati ya hao uliowaandika ila unachokiona kama ni uwezo wao mkubwa wa akili wameumbiwa na mtunzi pamoja na director wa hiyo series. Mfano Michael Scofield, amembwa kama mtu mwenye ujuzi mkubwa katika fani ya uhandisi na unaweza ukadhani amesoma na kuhitimu shahada ya juu ya Uhandisi. Ina ukweli ni kuwa . "He graduated from
Princeton University completing his
bachelor's degree in
English Literature". source:
Wentworth Miller - Wikipedia, the free encyclopedia. Mi ninacho weza kuchangia hapoa ni kuwa hao jamaa wote uliowaandika hapo juu wanauwezo mkubwa sana wa kuigiza, ila pamoja na uwezo huo wameza kuupiga msasa au kukipiga msasa kipaji chao walicho nacho kwa kwenda shule and therefore their talent is supplemented by their educational background. Kitu ambacho ni nadra sana kukikuta kwa waigizaji wetu wa Nyumbani. Hebu fikiria mtu kamaliza darasa la saba alafu unampa scene ambayo itamkata yeye aigize kama lawyer...Hata iweza hata kama atahudhuria mahakamani mara mia ili kujifunza kile mawakili wanacho kifanya. Alafu kitu cha pili ni kuwa wenzetu wale wanavyoigiza hujua kama wanaigiza unaona kama ni uhalisia na ndio maana unaweza kuhadaika kuwa Scofueld ni Mhandisi kumbe sio. Ila huku kwetu mtu anaigiza afu anaigiza kuigiza...unamwona kabisa jamaa anaigiza hapa. Tunasafari ndefu waungwana