BRAKE kupata moto..

Mother Confessor

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
18,677
Reaction score
45,532
Hi,.hope weekend iko njema...

Tangu wiki iliyopita nikiwa road,nikikanyaga brake nahisi umoto kwenye nyayo na joto hupanda kadri ninavyokanyaga brake,.nimeogopa hata sielewi shida ni nini...

Nilipeleka kwa fundi wetu kitaa naona bado hali iko vilevile...nimeamua kuliacha kwa muda naogopa kulipukiwa...najua wataalam humu mpo naomba hata ushauri tuu tatizo laweza kuwa ni nini,au fundi/garage ipi nzuri tatizo hili likaisha kwa maeneo ya Dar..

Aina ya gari ni toyota allion..


Shukrani.
 
Master cylinder itakuwa inashida mara nyingi raba zake zikiisha inatokea hivyo tafuta mafundi wazuri wapo watakusaidia hilo ni tatizo dogo sana
Ahsante chief,.tatizo mafundi wetu uchwara wanakuza tatizo mpaka unaona bora uliache kwa muda...

Ahsante kwa ushauri.
 
Ahsante chief,.tatizo mafundi wetu uchwara wanakuza tatizo mpaka unaona bora uliache kwa muda...

Ahsante kwa ushauri.
Mafundi uchwara tatizo likiwa dogo watajifanya daaah!!! Aisee!!! Daah!!! Em ngoja kwanza!!!! Ataingia chini ya uvungu na hapa na pale na kijasho kinamtoka huku mwenye chombo unasema kwa tatizo hili niandae 50k hapa.kumbe ni jambo la kufanyiwa bure tu kulipa ihsani.

Ila sina gari hivyo napita kimya kimya tu mother.tusubiri wajuvi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahah me nishaambiwa hapa tatizo dogo hilo,.sasa ole nikaambiwe bei za ajabu,.ntapanda daladala tuu kwakweli kwani shin'ngapi😃😃
 
Piston za zinajaamu,peleka kwa fundi afungue matairi aangalie wheel cylinder,ina maana ukikanyaga break ukiachia piston hazirudi so zinasababisha hilo joto

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsanteni jamanii,.hapa napata hata nguvu ya kumtishia fundi kuwa najua tatizo lilipo😃 maana nilikuwa sijui A wala Z angenidanganya chochote ningekubali tuu..
 
Ahsante chief,.tatizo mafundi wetu uchwara wanakuza tatizo mpaka unaona bora uliache kwa muda...

Ahsante kwa ushauri.
Tafuta fundi/gerage moja tu ambayo utakuwa unatengeneza gari yako hapo itakuwa rahisi kufahamika na sometimes itakuwa ngumu kukupiga bei...

Nakushauri acha kutumia hizi brake fluid za 2000/= ni mabovu mno mafuta haya yanasababisha raba kwenye cylinder kuungua na zinakatika baada ya muda mfupi
 
Nitafanya hivyo,.ahsante sana👏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…