Branch Davidians lilikuwa kundi la kidini lililojiengua kwenye dhehebu la Ki-adventist baada ya Bwana Houteff kupishana na viongozi wa kisabato kwenye mambo fulani fulani. Kundi hili lilianzishwa na Victor Houteff mwaka 1935 hii ni baada ya machapisho yake aliyoyaita Fimbo ya mchungaji (Shepherd's Rod) kukataliwa. Hivyo aliona hakukuwa na namna ilimbidi kujitoa kwenye dhehebu lake la kisabato.
Machapisho ya Fimbo ya mchungaji yalikuwa yakitaka kufanyika kwa mabadiliko ambayo licha ya kutowekwa wazi yalipingwa vikali na viongozi wa Ki-adventist. Baada ya kujiengua, Victor Houteff alielekea eneo la Waco, Texas na huko ndiko kulikozaliwa kikundi cha Branch Davidians akiwa na watu wengi ambao nao walimfuata yeye. Na walikuwa wakikaa kwenye jamii yao waliyoipa jina la Mount Carmel Center
Ilipotimia mwaka 1955, Houteff alipoteza maisha na hapo kundi lote likaachiwa chini ya aliyekuwa mke wake Bi. Florence Houteff. Bibie huyu yeye alikuwa akijihusisha na utabiri juu ya mambo ambayo yangetokea dunia inapokaribia mwishoni (Apocalyptic Prophecies), kwa bahati mbaya mpaka kufikia mwaka 1959, tabiri zake zote hazikutokea kama alivyotabiri.
Mwaka 1957, akiwa bado kiongozi wa jamii ya Mount Carmel Center aliamua kuondoka na kusogea maili ishirini na moja kutoka Waco, Texas na kuelekea Elk, Texas na huko alinunua ekari 941 (941 acres) na kuanzisha jamii mpya aliyoipa jina la New Mount Carmel Center. Maamuzi ya kuamia Elk, Texas yalitokana na kutoelewana kwake na kiongozi mpya ambaye alijitangaza kama "mjumbe maalum" wa Mungu kwa jamii hiyo aliyefahamika kwa jina la Benjamin Roden. Benjamin Roden alikuwa akishirikiana na Lois Roden na George Roden
Benjamin Roden alikuwa mfuasi wa Houteff na aliishikilia imani ya mwalimu wake kiimani, huyu alipata nguvu mno na ushawishi na ukizingatia kufeli kwa utabiri wa Bi.Florence basi alijikuta akipata watu wengi. Baada ya muda Bi.Florence aliuza hata ile ardhi aliyoinunua kule Elk, Texas na kubakiza 77 acres pekee na kubaki na wafuasi wachache ambao bado walikuwa wakimuamini.
Fast forward baada ya muda jamii ya Mount Carmel Center ilipata kiongozi mpya aliyefahamika kwa jina la Vernon Howell almaarufu kwa jina la David Koresh, huyu aliamia kwenye jamii ya Mount Carmel Center na alijifunza mafunzo ya Biblia kutoka kwa Lois Roden. Baada ya mafunzo aliamua kujitenga na kuanzisha kundi lake la Branch Davidians Seventh Day Association na kundi hili lilikuwa likipingana na kundi lililokuwa linaongozwa na akina Roden. Kwa mara ya kwanza Koresh aliwafuata wakina Roden mwaka 1981 na hiki kilikuwa kipindi alipoenda kujifunza kwa Lois Roden ambaye aliishia kumgeuka. Kundi la akina Roden lilifahamika kwa jina la The Brach Davidians
Mwaka 1987 Lois Roden alifariki, kundi la Branch Davidians likabaki kwa George Roden. Baada ya kuona Lois Roden amefariki Koresh alijitangazia urais na alitaka haimiliki jamii nzima iliyotokana na Houteff bila kujali ilikuwa chini ya viongozi gani kwa muda huo. Koresh aliifuata jamii ya Branch Davidians na kuwavamia na hapo walipigana risasi ilimradi tu apate madaraka na kumng'oa George Roden aliyerithi Uongozi kutoka kwa Lois Roden. Hii ilikuwa mwaka 1987
Mzozo huo ndio uliopelekea mapigano ya siku 51, ambayo yalisabaisha eneo la Waco, Texas ambako wafuasi wa George Roden kuwaka moto ambao mpaka sasa haijulikani ulisababishwa na nani kati ya maafisa wa Polisi na waumini wa The Branch. Hii ilikuwa mwaka 1993, mapigano haya ya 1993 yaliwaingiza maafisa wa Serikali katika ngazi ya Ulinzi kuzuia mpambano ule ambao haukuonekana mwisho wake.
Katika mapambano ya 1993 ndani ya siku 51 maafisa wanne wa Bureau of Alcohol, Tobacco and Firearms (ATF) walipoteza maisha. David Koresh alipoteza maisha baada ya kidonda chake cha risasi aliyopigwa kichwani katika utekaji wa Waco kupelekea umauti wake. Mwili wa David ulikutwa Mount Carmel Center kwenye kaunti ya McLennan huko huko Texas
Fast forward mpaka mwaka 1995, mwaka huu veteran mmoja wa vita vya guba (Gulf War) aliyekuwa akifahamika kwa jina la Timothy James McVeigh aliamua kulipa kisasi cha roho za watu waliopotea katika uvamizi uliofanywa na Serikali ya Marekani katika eno la Waco. Huyu mzaliwa wa Lockport, New York aliyekuwa na majina mengi kama Tim Tuttle, Robert Kling na Darly Bridges alikuwa akifanya kazi ya Ulinzi kabla ya kulipa kisasi.
Ilikuwa majira ya saa tatu asubuhi April 19, 1995 Timothy McVeigh akishirikiana na Terry Lynn Nichols walilipua bomu maeneo ya Oklahoma. Bomu hili liliua watu 168 na kusababisha majeruhi ya watu 680. Tukio hili linakumbukwa kwa jina la Oklahoma Bombing na lilisababisha hasara ya dola za kimarekani milioni 652 ($652 million). Timothy McVeigh aliuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu kama hukumu yake iliyopitishwa na mahakama na Terry yeye amefungwa kifungo cha maisha mpaka leo hii na hawezi kupewa msamaha wa aina yoyote.
Till next time
PHOSGENE