Kwani hujui kama mchezo wa kubet unachezwa na wengi ikiwemo makocha, marefa na wachezaji? Trend ya matukio ilikuwa inaonesha wazi kuwa Constantine ndiye atakayeshinda mchezo..... na kitendo cha kupindua meza kibabe magoli mawili refa akaona mkeka unatiki huu. Ilivyoingia goli kwa Bravo kumemchanganya ikabidi asikilizie.....
Ni sawa sawa na refa aliyechezesha mechi ya Simba... Kaona move ya goli kwa Simba na Che Melon kaishaachwa akapuliza filimbi ya faulo badala ya kuacha advantage. Che Melon ni mtu wa mwisho na amefanya faulo ya makusudi kuzuia mpinzani kufunga lakini kampa njano badala ya Red.
Dakika zimeongezwa 7 na bahati nzuri ndani ya zile dakika 7 hakuna mchezaji wa CS Sfaxien aliyedondoka wala wa Simba, mpira muda wote langoni mwa CS Sfaxien tu hakuna kumpumzika, lakini refa zinafika dakika 8 yeye anachezesha tu na hata dalili ya kuangalia saa hana, aliibetia Simba yule.
Dakika huwa ni za wote lakini kwenye mpira yule anayenufaika na sare au ushindi, anatamani mpira uishe chap tu.