Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Huenda Brazil ikapoteza haki ya kura katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa kama itashindwa kulipa mchango wa lazima wa uanachama inayodaiwa kufikia mwishoni mwa mwaka.
Brazil ipo hatarini kupoteza haki ya kura katika baraza kuu la Umoja wa Mataifa kama kufikia mwishoni mwa mwaka huu itashindwa kulipa mchango wa lazima unaotolewa na kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Mataifa ambao una nchi wanachama 193, katika miaka 10 ya hivi karibuni umekuwa ukikabiliwa na changamoto kubwa ya bajeti. Kufikia sasa nchi wanachama 54 hazijalipa michango. Brazil inadaiwa na Umoja huo zaidi ya dola milioni 415.
Kwa mujibu wa ibara ya 19 ya sheria za Umoja wa Mataifa nchi mwanachama inaweza kupoteza haki yake ya kura kama ikishindwa kulipa michango ya lazima kwa zaidi ya miaka 2.
Baada ya Marekani nchi ya 2 ambayo inadaiwa deni kubwa zaidi na Umoja wa Mataifa ni Brazil. Ili Brazil isipoteze haki hiyo inapaswa kulipa dola milioni 126 mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka.