Brazil: Mama amuua mtoto wake kwa sababu ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Tatiana Pereira amehukumiwa jela miaka 25 na miezi nane kwa kumuua makusudi mwanae wa kiume aliyefahamika kwa jina la Lozano (17) kisa ni shoga ambapo hakupendezwa na sexuality ya mwanae huyo.

Awali, mwanamke huyo aliwakodi jamaa wawili kwa majina ya Victor da Silva na Miller da Silva Barissa ili wamuue mwanae huyo. Jamaa hao(thugs) walimshushia kichapo kijana huyo hata hivyo walighairi kumuua ambapo mama mtu kuona hivyo alimua kuingia mwenyewe mzigoni kummaliza kumtoa uhai mwanae.

Akiwa Mahakamani mwanamke huyo amekiri kuua, lakini amepinga kumuua mwanae sababu ya kuwa shoga kwa kudai mwanae huyo alimtishia kumuua ndipo akamuwahi yeye.

Hata hivyo, Daria, baba mdogo/mkubwa wa Lozano akihojiwa na kituo cha TV nchini humo amempinga shemeji yake huyo kwa kusema, Lozano alikuwa ni kijana mpole, mwenye heshima na msikivu pia tayari alikuwa anafanya kazi, isipokuwa tatizo lake ni hiyo sexuality yake na siku zote mama mtu hakupendezwa na ndio sababu ya kumuua

Kwa upande mwingine jamaa waliokodishwa kumuua wao wamehukumiwa jela miaka 21 na miezi nane.
 
He he! Ambacho sikielewi hapa ni hiyo mahakama inatetea uhai au ushoga au vyote viwili!!!!
Waafrika tukopi Mambo ya maana lkn mengine tuwaachie wenyewe wenye mahakama za haki.
 
Mashoga bwana eti "seuality yake". Ushoga ni sexuality au ni upuuz wa mfirwaji tu??

Back
Top Bottom