Hakuna ku guess kuhusu mahakama zetu, chochote kinachoihusu serikali inayowapa hizo kazi na kula tunafahamu wataitetea serikali yao.Walalamikaji wasije sema au kusingizia kwamba hawakuambiwa... kutokwenda mahakamani Kwa kisingizio chochote kile ni ku- second guess maamuzi ya mahakama ambayo hatujui itaamua nini hii test kesi ikifunguliwa...
Wamewahi kuambiwa, hawana ukubwa wowote ikiwa mlipaji wa pesa za mishahara na uendeshaji wa mahakama zao ni mtukufu rais.
Na mtukufu rais aliwaambia hawako independent ikiwa kila kitu wanamtegemea yeye, anawateua, anawajengea majengo, anawateulia jaji kiongozi, anawateulia mwanasheria mkuu wa serikali, anawateulia waziri wa sheria na katiba, hivyo kwa kufupisha maelezo, wanapaswa ku act in favor of serikali iliyopo, na siyo hiyari kwao kuitetea serikali ni lazima, hakimu au judge asiyetaka kufanya hivyo kwa kujidai yuko neutral aliambiwa aondoke awekwe mwana ccm, there is no neutrality ni ama uwe ccm au usiwe hakimu au jaji kwenye serikali yake mtukufu rais.
Hatuhitaji research ku prove hili, hata kwenye mtifuano wa CAG uliona nini kilifanyika, sasa nani anaweza kuthubutu kufanya otherwise?!
Ni yeye aliyeamua tujitoe mahakama ya Africa iliyopo nchi kwetu, baada ya kuona kule wanaamua kesi zao kwa haki, alipomteua jaji kutuwakilisha kule mahakama ya afrika yule mama walisema atatenda haki na watayakubali maamuzi ya mahakama ile, kesi ngapi ziliamuliwa mahakama ya afrika wakapewa nakala ya hukumu kutekeleza wakakataa?!
I always say, we have laws but no justice.
Mfumo wetu uliishaamua kuwa bias, linapokuja swala la justice, hasa kuihusu serikali iliyopo.
Timeona kesi za wafanyakazi wakiiangusha serikali lakini hakuna utekelezaji, akiamua haurudi kazini hata kama mahakama ya rufaa ikiamua urudishwe haurudi kazini, na itakuwa hivyo kwasababu kaamua yeye na hakuna wa kumfanya kitu chochote.
Nimewahi kuuliza, ikiwa mtu yuko juu ya sheria, lakini yeye ndiye mtunzi wa sheria zetu, na yeye ndiye jaji mkuu, yeye ndiye mwanasheria mkuu, yeye ndiye DPP, yeye ndiye mkuu wa magereza, kwa nini ana apa au kuapishwa?!
Kiapo kinafaida gani kwa mtu aliyeko juu ya sheria?!
Yani ni sawa kusema kwamba Mungu anaapishwa na malaika, wakati hawa malaika hawana uwezo wa kumuwajibisha Mungu, sasa kwanini ana apa au kuapishwa?!