Elimu ya Tanzania iliporomishwa mwaka 1967 tulipoamuwa kuwachana na mfumo uliowekwa na Waingereza. Kwa miaka 38 baada ya hapo tukajitahidi kufanya kila njia kuigaragaza elimu kwa wengi na kuwasomesha wachache ambao tulidhani wangeifanya kuwa hii nchi ni pepo ya dunia. Kwa bahati mbaya kabisa hao wachache waliosomeshwaa kwa makusudi kabisa, wakawa ndio kuni za kuiteketeza hii nchi katika kila nyanja, kuanzia elimu, afya, uchumi, utalii mpaka utu na jamii.
Leo miaka 7 ya Kikwete tunaona mabadiliko makubwa sana, tunaona vyuo vikuu vikijengwa kwa idadi ya zaidi ya kimoja kila mwaka toka aingie madarakani, tumeona shule za sekondari zaidi ya 4000 zikijengwa wakati wake, tumeona kuwa kuna baadhi ya shule wameruhusiwa wafate mfumo wa Kiingereza na kwa sasa unatambulika tena rasmi.
Tunaona jitihada na bajeti ya wizara ya elimu ikipanda kila mwaka. Ni mwanzo mzuri baadaa kusambaratishwa na kutuacha kuwa nchi ya mwisho kielimu kulingana na jirani zetu kama Kenya na Uganda.
Tunamtakia kila la kheri Kikwete airudishe mitaala na iwe bora kuliko ilivyokuwa wakati tunapata Uhuru.
Wengi tulioiwahi elimu na mitaala ya mkoloni tunasikitishwa sana tukiona elimu ilipopelekwa pabaya, sijui nani alitudanganya kuwa tunaweza kuleta maendeleao bila kuwekeza kwenye elimu kwa nguvu zaidi? Nakumbuka shule yangu ya awali Kisarawe, tulikuwa na kila cha kujivunia kama shule na nakumbuka shule yangu ya pili H. H. The Agakhan Secondary School ambayo baadae ikaja kuitwa Tambaza Secondary School.
Tulikuwa tuna maabara ambayo hata hospitali nyingi tu nyingine kwa sasa haina. Tulikuwa tuna Art room, ambayo ukiingia unajuwa nipo chumba cha ma artist. Tulikuwa tuna vifaa vya michezo ambavyo hata timu za Taifa kwa sasa hazina,tulikuwa,tulikuwa,tulikuwa,tulikuwa.Rohoinaumasana.