Breaking News: Hatimaye Rais wa TFF Jamal Emily Malinzi ameondoa jina na kukubali yaishe Urais TFF

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Habari za muda huu.

Taarifa ambazo nimezipokea japo kwa taabu na usiri mkubwa zinasema kwamba hatimaye Rais wa TFF Ndugu Jamal Emily Malinzi amekubali kuondoa jina lake katika Uchaguzi ujao wa TFF na ameamua kutogombea tena.

Inasemekana taarifa zote za kuhusu hili zitatolewa ndani ya Saa 24 au 48 zijazo kupitia kwa Wakili wake Mkuu na kwamba unasubiriwa tu Mkutano wa dharura wa TFF ambao unategemewa kufanyika Kesho ambao utajadili mambo mengi ila hili la Malinzi na Mwesigwa pamoja na Timu ya Taifa iliyopo Afrika ya Kusini katika michuano ya COSAFA ndiyo zitakuwa Agenda Kuu.

Narudia tena kusema kuwa hatimaye Rais wa TFF Jamal E. Malinzi ameamua kuondoa jina lake na kujitoa rasmi katika Kinyang'anyiro.

Ni hayo tu kwa sasa na nitarudi tena baadae muda wa Saa tano ( 5 ) kamili usiku tuendelee na mengineyo ila kwa sasa habari ni hii.

Kila la Kheri Ally Mayai na Mtemi Ramadhan.
 
Ila Ameondoka kwa kashfa Kubwa sana Duu Siju Kama Wambura naye ataendelea na Mpango wake wa Kugombea/..
 
[emoji16] [emoji16] [emoji16]

Kuna majamaa ya sheria yatakuja na vipengele vyao hapa,

Kuwa malinzi atagombea

[emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]

Afadhali [emoji109] [emoji109] [emoji109]
 
Afadhali labda taifa stars itakuja kubeba kikombe walau kimoja coz toka yupo huko mahabusu timu inafanya vyema alhamdulillah tumeingia nusu fainal kule south .......mungu ambariki kwa maamuzi yake
 
Angeendelea kung'ang'ania uRais wa TFF, lupango nayo ingemng'ang'ania. Sasa kakubali yaishe, mahakamani atapelekwa na dhamana itatoka.
hana dhamana labda afutiwe shitaka la kutakatisha ,kinyume na hapo awamu ya kwanza ya JPM ataimalizia segerea
 
Umhh tusubiri Huyo wakili wake
 
maji yamezidi unga. kaa mbali na watoto. hivi wakat wa kampeni za uchaguzi 2015 kama vile aliendaga kumsalimia-----------. Au hii ndo inayomgharimu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…