Breaking News:- Viongozi wa Uamsho wapewa dhamana

Breaking News:- Viongozi wa Uamsho wapewa dhamana

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
BREAKING NEWS............
VIONGOZI WA UAMSHO WAPEWA DHAMANA YENYE MASHARTI MAGUMU. WAREJESHWA RUMANDE

Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani

Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe ya mjini Zanzibar, leo imetoa fursa ya dhamana kwa Viongozi wa makundi mawili ya kidini Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa ya kufanya fujo na kupelekea ghasia na vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Watuhumiwa hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikhe, Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe, Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman na Hassan Bakar Suleiman.

Akisoma uwamuzi huo huku kukiwa na ulinzi mkali eneo lote la Mahakama, Hakimu wa Makahama hiyo Mh. Msaraka Pinja, amesema kuwa ingawa upande wa Mashtaka ulikuwa haukutoa pingamizi ya dhamana kwa watuhumiwa, lakini Mahakama ililazimika kusitisha utoaji dhamana baada ya kupitia mambo kadhaa ya msingi.

Amesema kuwa pamoja na uzito wa tuhuma zinazowakabili watuhumiwa, Mahakama ililazimika kusita kutoa dhamana kwanza kwa usalama wa watuhumiwa wenyewe na kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo na uwezekano wa kuingilia upelelezi wa kesi inayowakabili.

Hakimu huyo alisema wasiwasi wa Mahakama ilikuwa kwamba watuhumiwa hao wakiwa nje ya dhamana kuna uwezekano wa kutenda kosa lingine, Kutohudhuria Mahakamani kwa wakati wanapotakiwa na kuangalia kwa mapata uzito wa kosa wanaloshitakiwa nalo.

Baada ya kuridhika na Mahakama hiyo ilitoa dhamana kwa watuhumiwa wote saba kwa mashariti ya kuwasilisha mahakamani fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni tatu kwa kila mmoja pamoja na kuwa wadhamini watatu ambao ni watumishi wa Serikali kwa kila mmoja akitoa kiasi kama hicho cha fedha mahakamani.

Watuhumiwa hao pamoja na Wadhamini wao, kwa pamoja wametakiwa kuwasilisha barua kutoka kwa Sheha wa Shehiya anayoishi pamoja na kivuli cha vitambulisho vya Zanzibar Mkazi na kwa wale wenye Hati za Kusafiria pia wawasilishe vivuli vya hati hizo Mahakamani.

Pamoja na masharti hayo ya jumla, lakini pia wadhamini wometakiwa wawe watumishi wa serikali na wawakilishe barua kutoka katika ofisi wanazozifanyia kazi na vivuli vya vitambulisho vyao vya kazi ili view kama kumbukumbu mahakamani.

Hata hivyo watuhumiwa wote wamerejeshwa rumande baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana pamoja na kukabiliwa na kesi nyingine Mahakama Kuu ya Vuga, kesi ambayo dhamana yake imewekewa pingamizi kwa hati maalum ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar kwa sababu za kiusalama.
Kesi hiyo imeahirishwa tena hadi Novemba 21, mwaka huu itakapotajwa tena.

Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mmoja ya Mawakili wa Watuhumiwa hao Bw. Abdallah Juma, amesema yeye pamoja na wakili mwenzake Bw. Salum Toufik, wataendelea kuwatetea watuhumiwa hao hata baada ya kutishia kujitoa katika kesi hiyo mwezi uliopita.
 
Jela makazi ya wakorofi! Gvt has to be careful na hili zigo la Udini TZ!
 
Ni katika mahakama ya Mwanakwerekwe Zanzibar leo.
Viongozi wa Uamsho walifikishwa mahakamani na umapde wa mashtaka ukasema dhamana iko wazi na kutoa masharti.

Watuhumiwa hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikh Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikh MselemAli Mselem, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, KhamisAli Suleiman na Hassan Bakar Suleiman.

Awali Hakimu wa Makahama hiyo Mh. Msaraka Pinja, amesema kuwa ingawa upandewa Mashtaka ulikuwa haukutoa pingamizi ya dhamana kwa watuhumiwa, lakini Mahakama ililazimika kusitisha utoaji dhamana baada ya kupitia mambo kadhaa yamsingi.

Amesema kuwa pamoja na uzito wa tuhuma zinazowakabiliwatuhumiwa, Mahakama ililazimika kusita kutoa dhamana kwanza kwa usalama wawatuhumiwa wenyewe na kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo na uwezekano wa kuingilia upelelezi wa kesi inayowakabili.

Hakimu huyo alisema wasiwasi wa Mahakama ilikuwa kwamba watuhumiwa hao wakiwa nje ya dhamana kuna uwezekano wa kutenda kosa lingine, Kutohudhuria Mahakamani kwa wakati wanapotakiwa.

Na sasa dhamana iko wazi kwa watuhumiwa wote saba kwa mashariti ya kuwasilisha mahakamani fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni tatu kwa kila mmoja pamoja na kuwa wadhamini watatu ambao ni watumishi wa Serikali kwa kila mmoja akitoa kiasi kama hicho cha fedha mahakamani.

Watuhumiwa hao pamoja na Wadhamini wao, kwa pamoja wametakiwa kuwasilisha barua kutoka kwa Sheha wa Shehiya anayoishi pamoja nakivuli cha vitambulisho vya Zanzibar Mkazi na kwa wale wenye Hati za Kusafiria pia wawasilishe vivuli vya hati hizo Mahakamani.

washtakiwa wameshindwa masharti hayo na kurejea rumande hadi tar 21 Novemba

Picha hii Ikimuonyesha Sheigk Farid akirejeshwa rumande leo.
485111_304503159649780_2126761135_n.jpg
 
Mbona masharti ya kawaidia jamani hayo, ugumu wake ni hizo milioni tatu? sijaelewa kabisa hapa
 
Masharti hayo ya wadhamini wawe ni watumishi wa serikali halafu tena barua toka kwa mwajiri hilo limefanywa makusudi ili watumishi wataojaribu kuwadhamini waonekane nao ni uamusho na kuangaliwa na macho mawili!!!!
 
Mbona hela kidogo kwa Al-kaida hiyo!!!!?? Ha ha ha!!! Acha waendelee kula punje za jela!!! Tena ningekuwa hakimu ningesema kwa sababu ya kiusalama hawataruhusiwa kuletewa chakula toka nyumbani!!! Chezea serikali weye!!
 
wale wakereketwa na wapenzi wa uhamsho wakawape dhamana kwa maana kuongea ni bure kazi hiko kwenye matendo sasa..
 
wale wakereketwa na wapenzi wa uhamsho wakawape dhamana kwa maana kuongea ni bure kazi hiko kwenye matendo sasa..

na tuone huyo kiongozi wa serikali au mtumishi atakayewadhamini hawa jamaa
 
wale wakereketwa na wapenzi wa uhamsho wakawape dhamana kwa maana kuongea ni bure kazi hiko kwenye matendo sasa..

Umesoma habari yote au umepitia kichwa cha habari tu ili na wewe ujitokeze KIDOLE na watu wajue kama upo hapa! Mtoto wa nje ya ndoa hata ukimtia ndani ya Chupa ni lazima atajitokeza KIDOLE! Subiri kidogo na wengine watajitokeza muda si mrefu!.
 
kwa hayo masharti,inaonekana serikali tu ndio yenye uwezo wa kuwadhamini.!
 
Utasikia watu wanasema "Wamepewa masharti magumu kwa sababu ya mfumo kristo, na hakimu inaonekana pia ni chadema"! period!!
 
Mh raisi wa zanzibar
hao washenzi naomba dhamana yao wabongoe bila ngguo hata masaa sita ndio muwaachie else wakija muwarudishe huko rumande kama kawa mpaka watakapotimiza dhamana hapo juu hawana adabu kabisa wanadiriki kumchinja polisi mbwa kabisa
 
breaking news............
Viongozi wa uamsho wapewa dhamana yenye masharti magumu. Warejeshwa rumande

maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na taasisi za kiislamu na jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu zanzibar (jumiki) wakifanya matembezi ya amani

mahakama ya wilaya ya mwanakwerekwe ya mjini zanzibar, leo imetoa fursa ya dhamana kwa viongozi wa makundi mawili ya kidini zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa ya kufanya fujo na kupelekea ghasia na vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Watuhumiwa hao ni mwenyekiti wa jumuiya ya maimamu zanzibar sheikhe, faridi hadi ahmedi na mwenyekiti wa jumuiya ya uamsho sheikhe, mselem ali mselem, mussa juma issa, suleiman juma suleiman, azan khalid hamdan, khamis ali suleiman na hassan bakar suleiman.

Akisoma uwamuzi huo huku kukiwa na ulinzi mkali eneo lote la mahakama, hakimu wa makahama hiyo mh. Msaraka pinja, amesema kuwa ingawa upande wa mashtaka ulikuwa haukutoa pingamizi ya dhamana kwa watuhumiwa, lakini mahakama ililazimika kusitisha utoaji dhamana baada ya kupitia mambo kadhaa ya msingi.

Amesema kuwa pamoja na uzito wa tuhuma zinazowakabili watuhumiwa, mahakama ililazimika kusita kutoa dhamana kwanza kwa usalama wa watuhumiwa wenyewe na kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo na uwezekano wa kuingilia upelelezi wa kesi inayowakabili.

Hakimu huyo alisema wasiwasi wa mahakama ilikuwa kwamba watuhumiwa hao wakiwa nje ya dhamana kuna uwezekano wa kutenda kosa lingine, kutohudhuria mahakamani kwa wakati wanapotakiwa na kuangalia kwa mapata uzito wa kosa wanaloshitakiwa nalo.

Baada ya kuridhika na mahakama hiyo ilitoa dhamana kwa watuhumiwa wote saba kwa mashariti ya kuwasilisha mahakamani fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni tatu kwa kila mmoja pamoja na kuwa wadhamini watatu ambao ni watumishi wa serikali kwa kila mmoja akitoa kiasi kama hicho cha fedha mahakamani.

Watuhumiwa hao pamoja na wadhamini wao, kwa pamoja wametakiwa kuwasilisha barua kutoka kwa sheha wa shehiya anayoishi pamoja na kivuli cha vitambulisho vya zanzibar mkazi na kwa wale wenye hati za kusafiria pia wawasilishe vivuli vya hati hizo mahakamani.

Pamoja na masharti hayo ya jumla, lakini pia wadhamini wometakiwa wawe watumishi wa serikali na wawakilishe barua kutoka katika ofisi wanazozifanyia kazi na vivuli vya vitambulisho vyao vya kazi ili view kama kumbukumbu mahakamani.

Hata hivyo watuhumiwa wote wamerejeshwa rumande baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana pamoja na kukabiliwa na kesi nyingine mahakama kuu ya vuga, kesi ambayo dhamana yake imewekewa pingamizi kwa hati maalum ya mkurugenzi wa mashtaka zanzibar kwa sababu za kiusalama.
Kesi hiyo imeahirishwa tena hadi novemba 21, mwaka huu itakapotajwa tena.

Akizungumza mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mmoja ya mawakili wa watuhumiwa hao bw. Abdallah juma, amesema yeye pamoja na wakili mwenzake bw. Salum toufik, wataendelea kuwatetea watuhumiwa hao hata baada ya kutishia kujitoa katika kesi hiyo mwezi uliopita.

mkuu bbj
niulzie hakimu ameoa??nataka kumwozesha bila dhamana wa masharti nafuu yeye tu atafute tkt ya ndege nampelekea dada ngu kwa kweli ///
 
hawa jamaa hawaaminiki,ndio maana hata matajiri wa kiislam wameogopa kuwadhamini.
Ngoja tuone mfadhili mkuu wa ugaidi na uhuni (walio ndani sio waislam ila wahuni na magaidi wanaojificha kwenye kivuli cha dini) Ibrahim Haruna Lipumba atawatoa lini
 
Back
Top Bottom