Breaking news!!!!!!!!!!

Dmussa,

Mimi sio msemaji wa Diallo au kampuni yake kwahiyo ukisema hawana ni makosa mno unless umeenda BRELA na kukuta info kama hiyo haipo.

Nilichosema mimi ni tofauti na hiyo basic info ambayo unaongelea.

Kampuni hizi za ndege mara nyingi huwa wanakodisha ndege na hivyo kuwafanya wawe na fixed assets kidogo sana. Mara nyingi pesa unayodeclare BRELA ni hiyo ambayo unaweza kusema assets (fixed and current).

Wanapojaza mtaji BRELA wanaweza kuweka pesa kidogo sana, huwezi kupata ukweli wote kwa kutumia info ya BRELA na ndio maana nikakuambia hizo ni internal information.

Ukiniuliza mambpo ya DM Investment mimi siwezi kujua, ni sawa na kusema kompyuta za IBM zimeenda wapi? Kila product au technology ina wakati wake. Haina maana kuondoka kwenye soko moja na kuhamia kwingine ina maana umeshindwa biashara.

Watanzania tuko negative mno na kila kitu, matokeo yake wote tunakuwa MAJUHA huku wageni wanachukua nchi.

Hata kama ni ufisadi basi afadhali fisadi Mtanzania anayewekeza Tanzania kuliko hao wanaokuja kuficha fedha Ulaya.
 
Watanzania tuko negative mno na kila kitu, matokeo yake wote tunakuwa MAJUHA huku wageni wanachukua nchi.

Hata kama ni ufisadi basi afadhali fisadi Mtanzania anayewekeza Tanzania kuliko hao wanaokuja kuficha fedha Ulaya.

I didn't say I'm negative about Diallo Mkuu, I said he seems like his Homework was'nt done well hivi hakuwa na Internal Auditor(Risk analyst). There is no point kuanzisha such a CAPEX project and let it die after a few months?? Hivi hata Break Even point aliifikia au ndio iko 5yrs to come????

Kwangu kuwekeza bongo ni jambo la maana sana ila nashindwa kuelewa upeo wetu katika kuwekeza uko wapi...labda mkuu unisaidie katika hili.
 

Mkuu DMussa,
Mimi nadhani ukisoma vizuri sababu walizotoa Community Airline ni za msingi.
1. Cost ya wet lease ilikuwa kubwa na wameweza kupata vendor mwingine ambaye anaweza kusupply hizo ndege tena kwa dry lease at half price with better terms including your own pilots. Sasa huoni kuwa huo mkataba wa kwanza haukuwa mzuri na kama any dynamic businessmen decision waliofikia ni sahihi kabisa.

Biashara yoyote lazima ujaribu kwanza sasa kama Community Airline wamejaribu na kuona kuwa Price Leadership strategy/Low Cost Producer( By Professor Michael Porter in his book Competitive Strategy))inafaa kwenye Aviation Industry hapa kwetu kwanini wasijipange upya katika kupunguza cost.Wewe huoni kuwa Risk Analyst mzuri ameweza kuona hili

Mi nadhani tuwaombee heri warudi salama ila wasikimbie kama wale wa NICO(Tanzania One).

Vilevile mkuu kufikia break even point lini ni uamuzi tu waliowekeza na kwa Industy kama ya Aviation sio rahisi hivyo. Kwahiyo hata kama wameproject after 5 years huo ni uamuzi wao na besides wanaweza wakaamua hivyo ila kuua upinzani tu alafu ndo wanaanza kazi ya kutengeneza faida.

Mimi nawapa BIG UP Community Airline, maana kuanzisha shirika la ndege na kuanza kuwapeleka mswaki ATCL na Precision si Mchezo,tena kwa kipindi kifupi hivyo.Je wengi wetu humu tunaweza kuanzisha biashara of that magnitude????


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…