Breakup ya kwanza ilikuaje?

de Gunner

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
2,044
Reaction score
4,558
Mwaka jana mwishoni niliexperience hio kitu, asikwambie mtu. Acheni mapenzi yawe kitu chenye nguvu kubwa duniani. Mimi nimekua nikiona watu wanalizwa na mapenzi, ila niliwachukulia wanyonge wa hisia na kuwaona wajinga kulilia mtu mwingine. Nilikua nasema huku nikijihisi ushupavu kua kamwe sitofanya huo uzembe.

Nimedate na wasichana kibao, ila hata kama tukiachana si feel ile sense nimepoteza kitu, labda sikupenda nilitamani who knows? Ila kamwe sikuwahi kuumia. Nilisikitika for maybe 2 days hivi then imepita hio, harakat za kusaka mwingine zinaanza.

Ila huyu msichana, sjui tu... labda nafsi ziligongana. Wakuu, omba yasikukute, alaf mapenzi sjui yapoje? It comes when you least expect, and goes when you need it the most. Sijawahi pitia maumivu makali kiasi hiko. Sikuhizi hata nikiona mtu kadata kwenye mapenzi simshangai.

Miezi almost 2 naugulia maumivu makali, nilikonda ndani ya 2weeks🤣. Asee mda mwingi namuwaza yeye tu, na kwa vile nilitaka yaishe kabisa mm huwa sipendi kwenda back and forth, napenda uwazi kama mtu ataonesha tofauti napenda kwenda straight. Ila kwa huyu mtu nilikua kama zoba vile, yaani makosa afanye yeye mimi ndo wa kuomba samahani. Ilifika kipindi nikasema enough. Alikua na jeuri coz alijua nimeoza.

So kuna siku nikasema nakiwasha, akiwaka fresh maana am not a slave. Tukawakiana then ukawa ndo mwisho, nilifanya makusudi ili nijiengue kwenye hilo tanuri la moto ingawa nilijua fika kabisa itaniumiza for so long.. Guys, ile week ya pili 2 niliisha sana, nilipoteza maana ya maisha bcoz yeye pia alikua na sehemu kwenye maana hio.

Mawazo mtiririko kama mfereji wa maji yalipita endlessly kwenye ubongo wangu kutwa kucha kumuwaza yeye. Huyu msichana alinifanya nisilale masaa 8 kama mwanadamu wa kawaida. Msosi haupandi, nikakosa interest kwenye hobbies maana it was fun alipo kuwepo. Basically maisha yangu yakawa stagnant. Ikawa ni cycle ya kuamka, kwenda kazini, nikirudi ntazuga naangalia movie mpk macho yaume maana nikisema niende kulala tu, naanza kumwaza, hapohapo ntaanza kuumia moyo. So nilijiforce kuwa busy to mda uende siku iishe nianze cycle upya. Inshort skutaka tena mahusihano na mtu mwingine. Mpk hapo baadae nilipo pona hayo maumivu ya kumpoteza huyo mrembo. Ilinichukua almost miezi 2 ku heal na kuanza kukubaliana na hali, kuwa maybe hakuwa fungu langu. L
kadri siku zilivyo kua zinaenda ni kama mzigo flan ulikua unashuka emotionally.... duuh stori imekua ndefu nitaweka mwendelezo nikipata time,


Vp wewe, uliwezaje ku overcome first breakup? Kingine kuna watu hawajawhi kupenda kweli, wao wanatamani kama mm nilivyo kua mwanzo so hawana experience ya kupenda kweli, kuna tofauti kubwa hapo. Naomba hicho kigezo kizingatiwe kwenye comments.
 
Bado una sonona.Kitu cha kueleza kwa aya mbili umetumia siku tatu?
 
Kwanini mliachana au uli amua kukiwasha. Kwanini
 
Ali niandikia sma ndefu ya break up.kusema ukwel siku ijibu hadi kesho..ichi kitu kili muuma sana asee hapa nili fanya comeback badala ya yeye kuni acha nkawa kama mimi ndo nme muacha[emoji28] maana ali irudia iyo sms kama mala 3 akizani labda ni mtandao sija iona aka tuma na whatsup nika bluetick.

Maumivu ya kuacha na kuachwa yana ka utofauti asee japo moyo uli niiuma ila nili kaza kiume. Baada ya kuachana utakiwi uonekane kama wewe ndo ulkua mnyonge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…