Breakup ya kwanza ilikuaje?

Breakup ya kwanza ilikuaje?

Mi wasichana wamtaani kwetu walikuwa wanadai bora wakae na magazeti kuliko kuwa na mahusiano na mimi (bonge la komwe halafu nilikuwa nimetitia,kafupii ,keusii).Hata huyu nilienae sasa hivi sijui kanipendea nini.Sina break up yoyote kwa sababu nilikuwa sitongozi .
 
Dah mie nadhani bado maana nimewza hapa idadi ya pisi nlizopukutisha na kupiga chini pamoja na zile zilizonipiga chini sijawahi umia zaidi ya mmoja tu ambaye siku tunalimana maneno ya kumwagana akaropoka kuwa mm sijui show na alikuwa ananivumilia tu...dah asikwambie mtu nliumia mwezi mzima badae nkasema ntamtokea tena Ili akiingia kingi aisome namba ila ndio hivyo alishastuka.Kifupi yule manzi ananiuma hadi Leo na Sio Kwa lingine bali neno lake like.
 
Break yangu ya kwanza ilikua 25 December 2009 jioni ya X mass kwa My first love na ndiye mwanamke wa kwanza kufanya nae mapenzi tuliachana baada ya kumfumania ndani na rafiki wa kaka yangu wanafanya mapenzi.

Then pale demu aliposema anampenda mchizi kuliko mimi jamaa alikua yuko njema tu kiuchumi kumbuka ni rika la kaka yangu na nilienda pale baada ya kutumwa na bro kufuata kisu maana tulikua tunakaa jirani kwa bahati mbaya hakua amefunga mlango ndo ikatokea hilo maana walikua wanafanya pale sebuleni. Hiyo siku nililia kama mtoto mdogo na ukaibuka ugomvi mkubwa kati ya kaka yangu na mshikaji wake baada ya miaka 3 ndo wakaumaliza ila aliniachia kovu yule mwanamke.

Break yangu ya pili hii ndo mpaka sasa inaniuma sana kuliko ya kwanza nilikutana na mtoto facebook mwaka 2012- hadi tarehe 16/01/2023 ilikua ndo mwisho wa mapenzi yale mazito ,yote naweza sahau ila kauli ya "HAKUNA CHOCHOTE NAJIVUNIA KUHUSU WEWE TANGU TUMEANZA UHUSIANO". Wakuu mpaka sasa wametokea wanawake mbalimbali wakunitongoza au kuonesha dalili ya kunihitaji tena wengine mpaka pesa nikikwama wnanisaidia ila still imekua ngumu tena kumatch na mwanamke. Nimetumbukia kwenye msongo wa mawazo sana.

NB:Mwanamke wa kwanza alikua mzuri balaa kuliko wa pili ila mpaka sasa huyu wa pili ndo alinivuruga zaidi.

Kwa mwanaume yoyote jitahidi sana kutafuta uchumi mwanamke akikutangulia hatua 10 mbele kwa uchumi hilo penzi halitasavaivu.

Anyway maisha lazima yaendelee.
 
Kwanini mliachana au uli amua kukiwasha. Kwanini
Ngoja ni rudi nyuma kidogo....

Baada ya kukutana na huyu mrembo kuna kitu nilihisi ambacho ni ngumu kueleza kwa lugha tulizonazo, ila kuna kama JE-DAVU flan nilihisi ambayo haielezeki... nimekumbana na pisi kali sana na tuliachana ila kwa huyu, nahisi upendo haukutokana na muonekano wa nje nahisi. Ingawa alikua kisu pia, so kama kawaida yangu sikutilia maanani hizo hisia nikawa najivungisha kama si care sana.

Siku 3 tu za kumjua nikama vile tumejuana maisha🤣 kulikuwa na chemistry flan ambayo ilinifanya nilewe kabisa nikawa vulnerable asee sikuwahi kujihisi nimependa kiasi kile, kwenye shoo nilijihisi peponi, hata productivity yangu kazini ilipungua sometime nadoji siendi nasingizia ugonjwa, ili tu nispend time naye. Mpk hapo mtu alikua haniambii kitu maana huu upendo ulikua next level..

Kupunguza stori, kwa mara ya kwanza nilihisi uhalisia wa kukutana na mtu sahihi. Wengine ilikua nikishaona ya ndani attraction kwisha. Ila huyu nilimpenda beyond that, nilitaka kabisa awe wa kufa kuzikana. Alinifanya nisiwe na tamaa tena, kwa madem wengine. She was my perfect match.

Ila wakuu kuna kitu kinaitwa right person wrong timing.. kuna vitu viko nje ya uwezo wetu. Sitaki kuexpose nini kilitokea mpk kuachana ila kaeni mki jua mpk mungu aamue huwezi kuwa na mtu sahihi. Mtu sahihi huja baadae kabisa mpk uwe emotionally strong kucontrol desires.

Nahisi labda hakuona intensity ya upendo nilokua nao kwake? Sijui, labda alipitiliza kupenda mpka kuumia? Maana upendo halisi hufungua moyo na kuufanya uwe vulnerable? (It opens old wounds!) Sijui ila ni dhahiri tulipendana. Ilikua kama addiction hata tukizozana asubuhi, jioni sex kama kawa... so mimi nilihisi hii itakua sio sawa. Ile jeuri ya kila mmoja wetu ilikua inatutafuna na nilitaka kuondokana na huu upendo wenye utamu na uchungu ndani yake. So nika end things japo nilijua kabisa itanichukua mda kuja ku get over her. Ilinifunza vitu vingi kujihusu na jinsi nilivyochukulia mahusiano na wanawake pia.
 
Ali niandikia sma ndefu ya break up.kusema ukwel siku ijibu hadi kesho..ichi kitu kili muuma sana asee hapa nili fanya comeback badala ya yeye kuni acha nkawa kama mimi ndo nme muacha[emoji28] maana ali irudia iyo sms kama mala 3 akizani labda ni mtandao sija iona aka tuma na whatsup nika bluetick.

Maumivu ya kuacha na kuachwa yana ka utofauti asee
Asikwambie mtu mpaka upitie.
 
Dah mie nadhani bado maana nimewza hapa idadi ya pisi nlizopukutisha na kupiga chini pamoja na zile zilizonipiga chini sijawahi umia zaidi ya mmoja tu ambaye siku tunalimana maneno ya kumwagana akaropoka kuwa mm sijui show na alikuwa ananivumilia tu...dah asikwambie mtu nliumia mwezi mzima badae nkasema ntamtokea tena Ili akiingia kingi aisome namba ila ndio hivyo alishastuka.Kifupi yule manzi ananiuma hadi Leo na Sio Kwa lingine bali neno lake like.
🤣🤣🤣 alikuwa aanataka akuumize huyo, usichukulie maanani.
 
Back
Top Bottom