Breakup ya kwanza ilikuaje?

Hahaaa nimecheka hapo kuna mzigo umekukwama kifuani.

Mi nipo chuo mwaka wa 3 SUA 2006, Nilipata Binti 1 wa kiruguru toka Nyandira huko. Akawa Demu wangu, nilimpenda sana yule binti naye alinipenda sana. Pamoja na kumpenda, nilikuwa mbabe sana kwake. Asipopokea simu au hata asiponitafuta ni ugomvi na vita. Yule binti aliniingia sana, ilikuwa ni lazima nimbipu naye anibipu tu hata kama hatuna la kuongea hii ni kuonesha tunapendana. Yaani kwa siku naweza mbipu mara hata 20 naye hata mara 20 basi tu kuonesha tunapendana na kukumbukana.

Akapata chuo kule Arusha Tech. Hahaaaa wajanja wakamjanjarusha, mawasiliano yakapungua na ukaribu ukaanza pungua. Akawa hapokei simu wala nibipu huku mi nakereketwa tokana na mazoea. Akarudi likizo Moro, kwenda kumuangalia kwao nikampigia kumbembeleza haipokelewi nikaja muona anaongozana na jamaa mmoja wakati huo hakuwa anapokea simu yangu.

Dah, nilipagawa na kuwa kama chizi. Kama sijanywa pombe kipindi kile, siji kunywa pombe tena maana jamaa tulikuwa tunasoma wote wakawa wananitoa out club na kumbi mbalimbali angalau nimsahau. Semester ile ya 5 nilishikwa ngoma 4 na nikapiga third attempt 2. Dah, alinitesa sana yule binti.
 
We acha tu mzee wangu, hawa wapenzi wetu wana waamini sana marafiki zao hasa kwenye mambo ya mahusiano yn wakikuweka kwenye mahakama yao ujue umeisha
Siku za mbeleni huwa wanakuja kujuta.
Anaweza kufika miaka 35 hajaolewa, anaanza kujutia ya nyuma. Karma inatenda hapo maana unakuta alikuacha kwa nyodo.
 
Rafiki yangu alifunga siku 70.Siku 40 za Wakristo na 30 za Waislamu.Pale kwenye watsapp yake palikuwa pameandikwa I'm strong enough to let it GO.Yeye ni mzee wa kuachwa tu .Alioa na mke nae kamuacha mwaka jana.Hakika mwamba aliteseka.Haka kastori nimekatunga tu kunogesha uzi.Usikazingatie.
 
Ilikuwaje hadi kukuacha na watoto? Ila watu wana roho mbaya loh
 
Siku za mbeleni huwa wanakuja kujuta.
Anaweza kufika miaka 35 hajaolewa, anaanza kujutia ya nyuma. Karma inatenda hapo maana unakuta alikuacha kwa nyodo.
Kuna mmoja aliniacha , kumbe kamvisha mdada mwingine Pete, .nikaja kuambiwa na rafiki zake. Ila haya maisha, wamekuja kuachana tena ndoa ya kanisani. Juzi juzi kanitafuta. Haya maisha bwana ni bora kumuambia mtu ukweli kuwa nina mtu mwingine kuliko kufanya maamuzi kimyakimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…