Breakup ya kwanza ilikuaje?

Breakup ya kwanza ilikuaje?

Kiliniramba alooh! Maji niliita mma, siku tatu nzima nilijifungia ndani, na repeat song ya pain in me kuanzia asubuhi hadi usiku..usiku wa manane. Nakumbuka watoto wanarudi shule jioni wanaona kama siko sawa." Daddy are you allright?!" .lilikuwa swali la watoto kila wanaporudi shule. Sasa sijui walizungumza nini na mama yao ( ex - wife ) akanitumia ujumbe angalau ulinipa nguvu na kuwaza kuwa inabidi nisimame imara. " alubati are you okay? Najua hali hii inaumiza lakini imeshatokea,hakuna kitu tunaweza badilisha,move on...stay strong..stay strong just for hao watoto,unawapa wasiwasi na unyonge pia." Kuanzia hapo nikawa kama nimezinduka usingizini. Hata aina ya mziki nikabadilli sasa kutoka why dont you see that pain in mee ...hadi ridin' ya chamilionare,nakumbuka nikiwa room na rap " they se me rollin' ..they hatin'.. patrollin tryna catch me ridin' dirty,tryna catch me ridin' dirty..
Nashukuru Mungu hili nalo lilipita salama.
Sasa hivi nikiwa na wapenzi watano naona wachache.
 
Mimi niliambiwa siendani nae hiyo ni baada ya kushauriwa na mashoga zake ety mimi sina swagga ety nanyoa kama babu, sivai pamba kali, nipo kama sipo 😂
Pole sana mkuu Mbaga Jr . Mimi nilipitia kama hii, ingawa sikuambiwa wazi wazi ila shoga zake ndio waliokuwa wanamshauri. Nikasepa zangu na ku-delete namba yake, cha ajabu hakufuta namba yangu akaanza kunitafuta tafuta kwenye simu nikawa na msimamo sikutaka kabisa kurudiana nae. Na hii kunitafuta ni baada ya yeye kugundua nilikuwa mtu mwema sana kwake.
 
Mwaka jana mwishoni niliexperience hio kitu, asikwambie mtu. Acheni mapenzi yawe kitu chenye nguvu kubwa duniani. Mimi nimekua nikiona watu wanalizwa na mapenzi, ila niliwachukulia wanyonge wa hisia na kuwaona wajinga kulilia mtu mwingine. Nilikua nasema huku nikijihisi ushupavu kua kamwe sitofanya huo uzembe.

Nimedate na wasichana kibao, ila hata kama tukiachana si feel ile sense nimepoteza kitu, labda sikupenda nilitamani who knows? Ila kamwe sikuwahi kuumia. Nilisikitika for maybe 2 days hivi then imepita hio, harakat za kusaka mwingine zinaanza.

Ila huyu msichana, sjui tu... labda nafsi ziligongana. Wakuu, omba yasikukute, alaf mapenzi sjui yapoje? It comes when you least expect, and goes when you need it the most. Sijawahi pitia maumivu makali kiasi hiko. Sikuhizi hata nikiona mtu kadata kwenye mapenzi simshangai.

Miezi almost 2 naugulia maumivu makali, nilikonda ndani ya 2weeks🤣. Asee mda mwingi namuwaza yeye tu, na kwa vile nilitaka yaishe kabisa mm huwa sipendi kwenda back and forth, napenda uwazi kama mtu ataonesha tofauti napenda kwenda straight. Ila kwa huyu mtu nilikua kama zoba vile, yaani makosa afanye yeye mimi ndo wa kuomba samahani. Ilifika kipindi nikasema enough. Alikua na jeuri coz alijua nimeoza.

So kuna siku nikasema nakiwasha, akiwaka fresh maana am not a slave. Tukawakiana then ukawa ndo mwisho, nilifanya makusudi ili nijiengue kwenye hilo tanuri la moto ingawa nilijua fika kabisa itaniumiza for so long.. Guys, ile week ya pili 2 niliisha sana, nilipoteza maana ya maisha bcoz yeye pia alikua na sehemu kwenye maana hio.

Mawazo mtiririko kama mfereji wa maji yalipita endlessly kwenye ubongo wangu kutwa kucha kumuwaza yeye. Huyu msichana alinifanya nisilale masaa 8 kama mwanadamu wa kawaida. Msosi haupandi, nikakosa interest kwenye hobbies maana it was fun alipo kuwepo. Basically maisha yangu yakawa stagnant. Ikawa ni cycle ya kuamka, kwenda kazini, nikirudi ntazuga naangalia movie mpk macho yaume maana nikisema niende kulala tu, naanza kumwaza, hapohapo ntaanza kuumia moyo. So nilijiforce kuwa busy to mda uende siku iishe nianze cycle upya. Inshort skutaka tena mahusihano na mtu mwingine. Mpk hapo baadae nilipo pona hayo maumivu ya kumpoteza huyo mrembo. Ilinichukua almost miezi 2 ku heal na kuanza kukubaliana na hali, kuwa maybe hakuwa fungu langu. L
kadri siku zilivyo kua zinaenda ni kama mzigo flan ulikua unashuka emotionally.... duuh stori imekua ndefu nitaweka mwendelezo nikipata time,


Vp wewe, uliwezaje ku overcome first breakup? Kingine kuna watu hawajawhi kupenda kweli, wao wanatamani kama mm nilivyo kua mwanzo so hawana experience ya kupenda kweli, kuna tofauti kubwa hapo. Naomba hicho kigezo kizingatiwe kwenye comments.
Mkuu,
Ume recovery within very short period of time ie. 2 months

Huwa inachukua muda Sanaa 😊 labda ukipata sababu mbaya mbaya za kumfanya umchukie

NB.
Love is wicked
 
Ali niandikia sma ndefu ya break up.kusema ukwel siku ijibu hadi kesho..ichi kitu kili muuma sana asee hapa nili fanya comeback badala ya yeye kuni acha nkawa kama mimi ndo nme muacha[emoji28] maana ali irudia iyo sms kama mala 3 akizani labda ni mtandao sija iona aka tuma na whatsup nika bluetick.

Maumivu ya kuacha na kuachwa yana ka utofauti asee japo moyo uli niiuma ila nili kaza kiume. Baada ya kuachana utakiwi uonekane kama wewe ndo ulkua mnyonge
Mwanamke ukimkaushia anaumia sana kwasababu anakosa attention yako. Safi sana mkuu.
 
Kazi zipi ? 😂weka yako kwanza
Za ujenzi wa taifa 😜

Mimi ukinitumia msg “ baby i love you 🥰” naisoma kwa dharau na kwa herufi kubwa tena kwa kisukuma “BEBI HAI LAVU YUHU👹” basi wala sikutilii maanani sasa hata ukiniacha ntaumia vipi??

Wewe kuanzia ss hivi anza kusoma msg kwa mtindo huo uone km utasumbuka kupenda hovyo 😂😂😂😂😂
Tatizo unasoma kwa hisia na kwa sauti ya mtumaji kwann mapenzi yasikutese??
 
Pole sana mkuu Mbaga Jr . Mimi nilipitia kama hii, ingawa sikuambiwa wazi wazi ila shoga zake ndio waliokuwa wanamshauri. Nikasepa zangu na ku-delete namba yake, cha ajabu hakufuta namba yangu akaanza kunitafuta tafuta kwenye simu nikawa na msimamo sikutaka kabisa kurudiana nae. Na hii kunitafuta ni baada ya yeye kugundua nilikuwa mtu mwema sana kwake.
We acha tu mzee wangu, hawa wapenzi wetu wana waamini sana marafiki zao hasa kwenye mambo ya mahusiano yn wakikuweka kwenye mahakama yao ujue umeisha
 
Mwaka 1964 naingia Tabora Boys nikakutana na Stella mtoto wa sekandi masta. Hata sijui ilikuwaje lakini aliponipiga chini kidogo niache shule aisee. We were just young innocent souls searching for our place in this vast universe. Dah! Mapenzi nyie acheni tu!
 
Jamaa alikua anaelezea mwanae alivyo uwawa hasa kipind kile shooting kwa Black American ilikua kawaida coz of racism. Sasa mm nilikua nachukulia maumiv aliyopitia najipa ilinipate motivation. Nilipiga gym ambayo mpk leo nawazaga hivi ulemoto nilitoleaga wapi🤣 hakika yule manzi alinibadilisha.

Favourite line ilikua
2:00 in tha morning and we still high ass*d out,
screeming thug till I die before I pass out.
Kuna ile ana sema blame to my mama, am a Black thug nigga ni , ni ipi 😀
 
Mwaka 1964 naingia Tabora Boys nikakutana na Stella mtoto wa sekandi masta. Hata sijui ilikuwaje lakini aliponipiga chini kidogo niache shule aisee. We were just young innocent souls searching for our place in this vast universe. Dah! Mapenzi nyie acheni tu!
Ile nyimbo ya Stella wa kenya ilikuwa ime toka wakati huo??🤣😂
 
Back
Top Bottom