brela wameshabadilika wanatoka analog kwenda digital
Pole mkuu, mimi yalinikuta pia. Nilifuatilia website yao nikajiaminisha najua cha kufanya. Nikatia timu kwenye ofsi zao. Nilipofika nikakuta mishemishe kibao, nilimwambia mlinzi kuwa nataka kufungua kampuni akasema kuna mtu ataweza kunisaidia kama ningehitaji. Nikamwambia nahitaji kwanza nionane na ofisa anieleze cha kufanya. Akanielekeza kwenye ofsi moja nikamkuta mbinti..Yule mdada akaniambia niandike barua kuomba jina halafu ndo nimfuate. Nilipomuuliza hilo jina litachukua siku ngapi, kaniambia; hadi wiki moja. Nikamwambia kuwa nimeshaangalia mtandaoni hilo jina halipo. Akajibu, bora uandike tu barua huenda wakawa hawajaliapload ila limeshachukuliwa.Hivi jamani sisi watanzania ni lini tutakua na utu? Sio kwa sababu nimekukuta ofisini ndio utumie fursa ya kunigeuza kitega uchumi.brlea pameoza,bila kutoa rushwa file lako litazungushwa na huta hudumiwa pamoja na kua mmeweka matangazo kama 1000 ya rushwa lakini mnanukaaaaaaaaa jamani hivi waziri gani anahusika na hiki kitaasisi jamani acheni kunyanyasa wanyonge walioamua kujiajiri na kutengeneza ajira kwa ajiri ya watanzania wenzao tusaidieni vizuri sisi ni ndugu zenu jamani sio wa nchi jirani
Hiyo yote ni politics na wanatafuta fursa za kuiba pesa uliza wamenunua shilingi ngapi hiyo system na mimi niko brela nafuatilia issue yangu leo ni wiki ya pili napigwa tarehe,kitu cha ku activate kwenye digital inachukua wiki mbili? Mkuu utamu wa ngoma ingia ucheze
Pole mkuu, mimi yalinikuta pia. Nilifuatilia website yao nikajiaminisha najua cha kufanya. Nikatia timu kwenye ofsi zao. Nilipofika nikakuta mishemishe kibao, nilimwambia mlinzi kuwa nataka kufungua kampuni akasema kuna mtu ataweza kunisaidia kama ningehitaji. Nikamwambia nahitaji kwanza nionane na ofisa anieleze cha kufanya. Akanielekeza kwenye ofsi moja nikamkuta mbinti..Yule mdada akaniambia niandike barua kuomba jina halafu ndo nimfuate. Nilipomuuliza hilo jina litachukua siku ngapi, kaniambia; hadi wiki moja. Nikamwambia kuwa nimeshaangalia mtandaoni hilo jina halipo. Akajibu, bora uandike tu barua huenda wakawa hawajaliapload ila limeshachukuliwa.
Nilipotoka kwa huyo mdada, mlinzi kanidaka tena. Kauliza, amekuambiaje? Nikamjibu, kaniambia niandike barua ya jina, majibu yatachukua kama siku tano. Akajibu, labda ukiwa na bahati ila sana sana wiki mbili. akaniambia, yule kijana akikufanyia ni siku mbili tu kampuni yako imesajiliwa. Nikashawishika.
Yule mlinzi kampigia huyo bwana mdogo. Doga kanichukua tukashuka ngazi mpaka ofisi fulani za wanasheria. Tukakaa benchi la kungojea huduma, dogo kaanza kunipa mchanganuo. Kutokana na kiingereza chake nikatambua hardly huyo dogo ni form iv. Kazi nzima ya name search, kuandaa memorandum na article of association atafanya kwa Tzs 500,000/= including gharama za mwanasheria. Baada ya hapo ndo nitalipia gharama za BRELA na TRA kulingana na ukubwa wa mtaji. Nilipomwambia document zote ninazo mi nahitaji afuatiliye, akasema ni ngumu anataka kila kitu afanye yeye. Nikamwangalia, nikajisemea kimoyomoyo, yaani na degree yangu nikulipe wewe 500,000/= kwa kwa kukopy na kupaste Memorandum? Tukaagana, sasa ni mwezi wa sita napiga business na kampuni sijasajili, nasubiri Brela ikianza kufanya kazi bila vishoka ndo nirudi tena....
Utendaji wa BRELA ni indication ya kushindwa kwa MKURABITA. Brela haikupaswa kuwa na ofisi moja, ilipaswa iwepo kila mkoa. Kuhusu vishoka, mimi nilipokuta tangazo la KISHOKA HATAKIWI nikajua wanamaanisha kinyume chake. Kama haitawezekana huifikisha brela kila mkoa basi itafutiwe ofisi jengo linalojitegemea. Wanasheria walioko hapo ushirika wengi wao ni mawakala wa vishoka tu.Wewe umewakilisha wachache wanaosumbuliwa,nimeshuhudia mtu kasumbuliwa good 8 month anaambiwa file halionekani,kuna vishoka wanaotambuliwa rasmi na Brela na ukipitia kwao file linapatikana ndani ya siku 1 lakini ukifuatilia wewe kila siku utaambiwa file halionekani,na kuta zao zimepambwa na matangazo kua msitumie vishoka,mimi sielewi hii serikali sikivu iko wapi,namna hii swala la ajira litaendelea kua gumu na ndoto kulitatua kadri tunavyojaribu kujikwamua sisi wenyewe tunarudishana nyuma huku mabwenyenye wakila kodi zetu ndani ya viyoyozi na wakipelekwa nyumbani kwa na ving'ola vya polisi......eti mana encourage wawekezaji kwenye uozo wa kufanya kazi namna ya Brela ? Mtasubiri miaka 1,000,000 mtaendelea kutumikia makampuni yaliyopo kama viongozi husika wasipoingilia hali ni ngumu,na takukuru wapo na wanajua na hawachukui hatua ......INAUMA SANAAAAAAA
Nini Brela LITA je napo kumeoza hatari adi receipt wanaandika za mkono hovyo kabisa.
Pole mkuu, mimi yalinikuta
pia. Nilifuatilia website yao nikajiaminisha najua cha kufanya. Nikatia
timu kwenye ofsi zao. Nilipofika nikakuta mishemishe kibao, nilimwambia
mlinzi kuwa nataka kufungua kampuni akasema kuna mtu ataweza kunisaidia
kama ningehitaji. Nikamwambia nahitaji kwanza nionane na ofisa anieleze
cha kufanya. Akanielekeza kwenye ofsi moja nikamkuta mbinti..Yule mdada
akaniambia niandike barua kuomba jina halafu ndo nimfuate. Nilipomuuliza
hilo jina litachukua siku ngapi, kaniambia; hadi wiki moja. Nikamwambia
kuwa nimeshaangalia mtandaoni hilo jina halipo. Akajibu, bora uandike
tu barua huenda wakawa hawajaliapload ila limeshachukuliwa.
Nilipotoka kwa huyo mdada, mlinzi kanidaka tena. Kauliza, amekuambiaje?
Nikamjibu, kaniambia niandike barua ya jina, majibu yatachukua kama siku
tano. Akajibu, labda ukiwa na bahati ila sana sana wiki mbili.
akaniambia, yule kijana akikufanyia ni siku mbili tu kampuni yako
imesajiliwa. Nikashawishika.
Yule mlinzi kampigia huyo bwana mdogo. Doga kanichukua tukashuka ngazi
mpaka ofisi fulani za wanasheria. Tukakaa benchi la kungojea huduma,
dogo kaanza kunipa mchanganuo. Kutokana na kiingereza chake nikatambua
hardly huyo dogo ni form iv. Kazi nzima ya name search, kuandaa
memorandum na article of association atafanya kwa Tzs 500,000/=
including gharama za mwanasheria. Baada ya hapo ndo nitalipia gharama za
BRELA na TRA kulingana na ukubwa wa mtaji. Nilipomwambia document zote
ninazo mi nahitaji afuatiliye, akasema ni ngumu anataka kila kitu afanye
yeye. Nikamwangalia, nikajisemea kimoyomoyo, yaani na degree yangu
nikulipe wewe 500,000/= kwa kwa kukopy na kupaste Memorandum? Tukaagana,
sasa ni mwezi wa sita napiga business na kampuni sijasajili, nasubiri
Brela ikianza kufanya kazi bila vishoka ndo nirudi tena....
hahaaaa: pole sn.
kwa hiyo umesusa kumalizia taratibu za usajili?
LITA ndo agency gani hiyo mdau?
Ipo hapa hapa Tanzania kweli?
Wanahusika na vizazi na vifo kama huna cheti cha kuzaliwa unapata huko
LITA ndo agency gani hiyo mdau?
Ipo hapa hapa Tanzania kweli?
Itakuwa RITA vizazi na vifo, kwa sasa wapo muhimbili, Pembeni ya Bilcanass kuna mjengo wao wa Ukweli unaendelea pale sijuhi wametoa wapi mabilioni yale.
Vizazi na vifo ni RITA, hao LITA wanahusika na bongo star search