Pole mkuu, mimi yalinikuta pia. Nilifuatilia website yao nikajiaminisha najua cha kufanya. Nikatia timu kwenye ofsi zao. Nilipofika nikakuta mishemishe kibao, nilimwambia mlinzi kuwa nataka kufungua kampuni akasema kuna mtu ataweza kunisaidia kama ningehitaji. Nikamwambia nahitaji kwanza nionane na ofisa anieleze cha kufanya. Akanielekeza kwenye ofsi moja nikamkuta mbinti..Yule mdada akaniambia niandike barua kuomba jina halafu ndo nimfuate. Nilipomuuliza hilo jina litachukua siku ngapi, kaniambia; hadi wiki moja. Nikamwambia kuwa nimeshaangalia mtandaoni hilo jina halipo. Akajibu, bora uandike tu barua huenda wakawa hawajaliapload ila limeshachukuliwa.
Nilipotoka kwa huyo mdada, mlinzi kanidaka tena. Kauliza, amekuambiaje? Nikamjibu, kaniambia niandike barua ya jina, majibu yatachukua kama siku tano. Akajibu, labda ukiwa na bahati ila sana sana wiki mbili. akaniambia, yule kijana akikufanyia ni siku mbili tu kampuni yako imesajiliwa. Nikashawishika.
Yule mlinzi kampigia huyo bwana mdogo. Doga kanichukua tukashuka ngazi mpaka ofisi fulani za wanasheria. Tukakaa benchi la kungojea huduma, dogo kaanza kunipa mchanganuo. Kutokana na kiingereza chake nikatambua hardly huyo dogo ni form iv. Kazi nzima ya name search, kuandaa memorandum na article of association atafanya kwa Tzs 500,000/= including gharama za mwanasheria. Baada ya hapo ndo nitalipia gharama za BRELA na TRA kulingana na ukubwa wa mtaji. Nilipomwambia document zote ninazo mi nahitaji afuatiliye, akasema ni ngumu anataka kila kitu afanye yeye. Nikamwangalia, nikajisemea kimoyomoyo, yaani na degree yangu nikulipe wewe 500,000/= kwa kwa kukopy na kupaste Memorandum? Tukaagana, sasa ni mwezi wa sita napiga business na kampuni sijasajili, nasubiri Brela ikianza kufanya kazi bila vishoka ndo nirudi tena....