Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza sana BRELA kwa maboresho katika utendaji kazi wenu mmekuwa active mno.
Baada ya pongezi nije kwenye hoja ya msingi ambayo imenifanya kuandika waraka huu ikiwa ni namna mnavyodeal na applications za registration ya makampuni.
Binafsi nimevutiwa na utaratibu mpya wa online registration umesaidia mno, Ila umekuja na changamoto zake.
1. Application kushughulikiwa na zaidi ya mtu mmoja.
Hili ni tatizo kubwa Sana na linapelekea ucheleweshwaji wa usajili kwa wakati.
Unapotuma application anayeipokea na kuifanyia kazi sio Yule Yule hii inapelekea mwendelezo kuwa wa kusua sua, huyu atakuambia lete hiki au rekebisha hiki, ukituma marekebisho anakuja mwingine kukuambia mengine ambayo wa Jana hakukuambia hivyo unaweza jikuta unapigwa Dana Dana hata miezi kadhaa.
2. Hakuna vigezo rasmi katika usajili.
Unakuta maombi ya Jana yamewekewa vigezo vyake.
Ukituma mengine kesho watakwambia vigezo vingine.
Kila Mara kumekuwa na vigezo mbali mbali ambavyo vinaleta usumbufu usiokuwa wa lazima kwa watumiaji wa mfumo.
Napendekeza yafuatayo:
1. Mgawanyo wa kazi,
Kwamba maombi yakishatumwa Basi aliyeanza kuyashughulikia aendelee nayo mpaka usajili utakapokamilika.
2. Vigezo vitavyofahamika na wadau.
Kwamba kwa kila category kuwe na vigezo Rasmi ambavyo kila mtu atapaswa kutimiza.
Au kunapokuwa na kigezo kipya taarifa zitolewe kwa wakati katika website yenu ili kila mtu ajue na avifuate kabla ya kupeleka maombi yake.
Otherwise kwa jinsi Mambo yanavyokwenda mdau anaishia kugombana na anaowahudumia au kushawishika kuwa mtoa Rushwa. Haipendezi kabisa.
Niishie kwa kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya na kuwaomba myafanyie marekebisho hayo niliyoyaainisha.
Kazi njema.