Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kwa kushirikiana na TISEZA @invest_in_tanzania na @sydf_tz , kimeendelea kuwajengea wanafunzi uwezo wa ujasiriamali na uwekezaji kupitia programu ya Public Lecture – Student Investor iliyofanyika kwa siku mbili, tarehe 30 na 31 Mei 2026 katika Ukumbi wa CIVE Auditorium.
Siku ya kwanza, tarehe 30 Mei 2026, wataalamu kutoka BRELA walitoa elimu kuhusu usajili wa majina ya biashara, usajili wa kampuni na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo.
Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Afisa Leseni wa BRELA, Bi. Winfrida Gaudence, aliwahimiza wanafunzi kushirikisha wenzao maarifa waliyoyapata na kuwapongeza kwa ushiriki wao mzuri.
Siku ya pili, tarehe 31 Mei 2026, wataalamu kutoka UTT AMIS walitoa elimu kuhusu uwekezaji, wakisisitiza umuhimu wa kuanza kuwekeza mapema hata kwa mtaji mdogo ili kujenga mustakabali bora wa kifedha.
Mafunzo hayo yamepokelewa kwa hamasa kubwa na wanafunzi, huku yakichangia kuwaongezea maarifa ya biashara, uwekezaji na ujasiriamali pamoja na kuwaandaa vyema kwa maisha na soko la ajira baada ya kuhitimu masomo yao.