Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Wakuu moja kwa moja kwenye mada bila kuwachosha.
Mimi siyo Chawa wala mtumishi wa BRELA. Mimi ni mdau tu mnufaika wa huduma za BRELA. Kwa wasiojua, BRELA ni Taasisi inayoshughulika na masuala ya usajili wa biashara /kampuni na kutoa leseni za biashara/kampuni nchini.
Mie nimekuwa mnufaika wa huduma zao rasmi kuanzia mwaka 2019. Sujui huko nyuma walikuwaje, ila kuanzia miaka hiyo ya 2019/2020 Kwakweli hawa jamaa wanastahili sana pongezi ukilinganisha na huduma za Taasisi nyingine za Bongo. Mie naelewa mazingira ya huduma nzuri yakoje katika nchi za dunia ya kwanza na huku kwetu dunia ya tatu. Hivyo nina maanisha ninapowapongeza hawa ndugu.
1) Hii Taasisi ime-digitalize huduma zake (kama siyo zote) online. Yaani unaweza kusajili kampuni yako na kupata leseni yako online bila hata kufika ofsin kwao.
2) Vilevile, ukishakuwa mteja wao, unaweza kufanya mabadiliko yoyote online bila kufika ofsin kwao kabisa.
3) Jamaa wapo active sana, yaani unafanya application leo, kisha kesho yake unapewa mrejesho wa jinsi gani ya kufanya marekebisho n.k.
4) Japokuwa changamoto yao ni kuwa kila huduma zao (iwe kusajili au kufanya any changes) lazima ulipie ila bei zao ni rafiki kwakweli.
5) Jamaa hawana bureaucracy kabisa, yaani taratibu zao ni short and clear. Zimenyooka kama rula.
6) System yao ya online si ngumu sana kutumia (ukilinganisha na wengine kama vile TANePS) kiasi kwamba mtu yeyote mwenye uelewa wa kuanzia hata kidato cha 6 hivi anaweza kutumia vizuri tu bila usumbufu.
Hongereni sana BRELA. Mnastahili pongezi nyingi sana. Natamani na Taasisi nyingine za Bongo kama vile TRA and the like zingeiga mfano kutoka BRELA, hakika tungekuwa mbali sana hapa Bongo.