KERO BRELA unaomba uthibitisho wa kampuni na unalipia lakini unaweza kusubirishwa wiki 2 hadi 3 bila sababu za msingi

KERO BRELA unaomba uthibitisho wa kampuni na unalipia lakini unaweza kusubirishwa wiki 2 hadi 3 bila sababu za msingi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,155
Reaction score
2,704
Huwa najiuliza unapokuwa unaomba mfano B.O au Custom Search ya kampuni kwa nini huwa wanazizuia muda mrefu? Muda ambao ukitoa "kipozeo" badala ya wiki 2 au 3 zinakuwa siku 2 au 3!

Kwanini siku moja tusiamke tukaamua wote tu tujenge taifa hili changa kwa pamoja kwa moyo wa dhati?
Ridhika na Mshahara tu hivi virushwa vidogo siku vitaku-cost upoteze nafasi.

Mtu kaomba form flani mtolee mpe halafu kubwa zaidi ni kwamba yule mtu atalipia na charge zinarudi serikalini pengine ndio zinatumika kukulipa wewe unae zuia hizo document na bado unataka akupe rushwa.

Tuliweka mifumo irahisishe na kuondoa huu urasimu lakini ni kama urasimu umeongezeka kwa hao wanaosimamia mifumo.
 
Ukishalipia unamtafuta mfanyakazi wao mmojawapo unamshikisha chochote unapata ndani ya 2 hours!
 
Hili tatizo hata RITA sipo sana eti wanatoa wiki 2 kufanya search ya ndoa unapotaka kufanya amendment ya makosa kwenye cheti cha ndoa iwe jina au shida nyingine
 
Ukishalipia unamtafuta mfanyakazi wao mmojawapo unamshikisha chochote unapata ndani ya 2 hours!
Hapa penyewe nimemshikisha lakini kupata hiyo control number ni msibaaa
 
Back
Top Bottom