BRELA wana tatizo gani ktk kusajili kampuni mtandaoni?

BRELA wana tatizo gani ktk kusajili kampuni mtandaoni?

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
12,675
Reaction score
25,924
Sio mimi tu, kuna ndugu zangu kama wawili wamesajili kampuni kwa njia ya mtandao, mwingine ofisini aliniambia alisajili jina la biashara, hela amelipia lakini hawafanyii kazi baada ya malipo, ukikaa muda fulani wanakuletea email kwamba application yako imekuwa cancelled, na maana yake na hela uliyolipa wamekula.

Wataalamu tuambieni, kuna shida gani au waseme tu watu tuwe tunafunga safari tunaenda jengo la Ushirika tukafanye manual, tuachane na hizi digital twende analogy.

Inakwaza kuona hili ni Shirika la Serikali, wafanyakazi wake ni wa Serikali, wanakula mshahara wa kodi zetu halafu wanaleta uzembe (sitaki kuita ujinga nitakuwa nimetukana).
 
Bongo na online wapi na wapi. Dirishani penyewe utasimama weee.
 
au wanataka tuwe tunawatumia pesa kwa mpesa za rushwa, haya mambo yataisha lini?
 
Siyo kwamba nataka kuwapamba, ila kwa maoni yangu, BRELA ni miongoni mwa TAASISI chache sana Bongo ambazo zipo well organized and digitalized. Huenda ikawa ni shida ya muda tu na wataitatua. Trust me, maana mie ni mteja wao tangu mwaka 2020 na sijawahi kujutia. Naomba unikopeshe imani yako katika hili. Mie siyo muimba mapambio, namanisha nachoongea. Kama kuna watu wengine kama mie wanaweza kuwa mashuhuda pia.
 
Upo sawa kabisa, katika hizi taasisi za serikali zinazotumia portal, BRELA ni wakongwe na wapo makini - ingawa bado wanahitaji kuongeza spidi. Wana sera yao kuwa maombi yanashughulikiwa ndani ya siku 3 za kazi, wajitahidi jambo hilo liwe kweli ndani ya siku 3 kivitendo. Changamoto aliyoipata mtoa mada inawezekana kweli kutokea, BRELA waitolee maelezo au wachukue hatua, maana kama hela imepokelewa maana yake ombi haliwezi kuwa na ukomo wa kufutika mpaka likamilike.
 
Mleta mada hata ukiwaita vyovyote sawa tu wewe ndio miongoni mwa waajiri.
 
Tuombe hao moderators watuwekee uzi wa brella ili tuhojiane nao humu humu
 
Brela wanajitahidi kwa kweli japokuwa sometimes huchelewesha kuthibitisha maombi ila kiasi fulani wanajitahidi. Kama kuna changamoto ulipata waweza kuiweka hapa ili tukusaidie kuitatua.
 
BRELA nawatetea. Hawana shida. Ukifika hatua ya kulipia hawawezi kukata application yako. Cha muhimu utimize vigezo.
 
Mnyonge mnyongeni, BRELA wana nafuu.

Hata customer care yao inajitahidi. Ukiwapigia wanatatua tatizo.

Japo sio kivile, lakini kwa levo za kibongo wana afadhali ukilinganisha na mataasisi mengine ya serikali.
 
Mleta mada ombi lako litakuwa na shida mahala, kwa uzoefu wangu tangu BRELA wameanza tumia PORTAL ufanisi umekuwa juu, hakuna delay za kipuuzi, plus hakuna tena rushwa kufanyiwa kitu BRELA.

Kwa aliyefanya kazi na ile BRELA ya analog ataleta ushuhuda humu, ili kazi yako ikamilike mapema kama huna chochote kitu, basi ingekuwa changamoto, BRELA ya leo wala hauhitaji kumjua mtu yoyote, unapata huduma za uhakika bila shida yoyote.

Kama una ombi lako kwa sasa na unaona linapata rejection kila mara, omba msaada wa mwanasheria, basi atatatua shida zako.
 
sio mimi tu, kuna ndugu zangu kama wawili wamesajili kampuni kwa njia ya mtandao, mwingine ofisini aliniambia alisajili jina la biashara, hela amelipia lakini hawafanyii kazi baada ya malipo, ukikaa muda fulani wanakuletea emial kwamba application yako imekuwa cancelled, na maana yake na hela uliyolipa wamekula. wataalamu tuambieni, kuna shida gani au waseme tu watu tuwe tunafunga safari tunaenda jengo la Ushirika tukafanye manual, tuachane na hizi digital twende analogy. inakwaza kuona hili ni shirika la serikali, wafanyakazi wake ni wa serikali, wanakula mshahara wa kodi zetu halafu wanaleta uzembe (sitaki kuita ujinga nitakuwa nimetukana).
Sio Brela tu mashirika na taasisi zote zinazotangazia watu eti watumie online tu.Hakuna kitu. Unachotaka hupati mpaka uende au uwatumie wafanyakazi wa ndani wenyewe. Ukiwa nje ukapata changamoto hawana sehemu ya kuchati moja kwa moja na hawajibu simu wala email..Mfano TBS wanakula pesa za watu kwa malaki na hawawasaidii watu kufanikisha biashara zao bali kazi kubwa ni kuwakwamisha kwa visingizio vidogo vidogo. Ingekuwa ni kama hivyo basi Uturuki isingeendelea kiuchumi na kiteknolojia.
 
Sio mimi tu, kuna ndugu zangu kama wawili wamesajili kampuni kwa njia ya mtandao, mwingine ofisini aliniambia alisajili jina la biashara, hela amelipia lakini hawafanyii kazi baada ya malipo, ukikaa muda fulani wanakuletea email kwamba application yako imekuwa cancelled, na maana yake na hela uliyolipa wamekula.

Wataalamu tuambieni, kuna shida gani au waseme tu watu tuwe tunafunga safari tunaenda jengo la Ushirika tukafanye manual, tuachane na hizi digital twende analogy.

Inakwaza kuona hili ni Shirika la Serikali, wafanyakazi wake ni wa Serikali, wanakula mshahara wa kodi zetu halafu wanaleta uzembe (sitaki kuita ujinga nitakuwa nimetukana).
1. Issue ya ombi kufutika ni pale ambapo ombi ambalo halikulipiwa linakaa kwenye mfumo kwa siku saba hapo litafutika.
Ombi ambalo limelipiwa linakaa kwenye mfumo kwa siku 365 kama lisipofanyiwa kazi linafutika.
2. BRELA haipo tena Jengo la Ushirika, imehamia Posta katika Makutano ya Mtaa wa Shaaban Robert na Sokoine Drive.
 
Back
Top Bottom