Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Upo sawa kabisa, katika hizi taasisi za serikali zinazotumia portal, BRELA ni wakongwe na wapo makini - ingawa bado wanahitaji kuongeza spidi. Wana sera yao kuwa maombi yanashughulikiwa ndani ya siku 3 za kazi, wajitahidi jambo hilo liwe kweli ndani ya siku 3 kivitendo. Changamoto aliyoipata mtoa mada inawezekana kweli kutokea, BRELA waitolee maelezo au wachukue hatua, maana kama hela imepokelewa maana yake ombi haliwezi kuwa na ukomo wa kufutika mpaka likamilike.Siyo kwamba nataka kuwapamba, ila kwa maoni yangu, BRELA ni miongoni mwa TAASISI chache sana Bongo ambazo zipo well organized and digitalized. Huenda ikawa ni shida ya muda tu na wataitatua. Trust me, maana mie ni mteja wao tangu mwaka 2020 na sijawahi kujutia. Naomba unikopeshe imani yako katika hili. Mie siyo muimba mapambio, namanisha nachoongea. Kama kuna watu wengine kama mie wanaweza kuwa mashuhuda pia.
Sio Brela tu mashirika na taasisi zote zinazotangazia watu eti watumie online tu.Hakuna kitu. Unachotaka hupati mpaka uende au uwatumie wafanyakazi wa ndani wenyewe. Ukiwa nje ukapata changamoto hawana sehemu ya kuchati moja kwa moja na hawajibu simu wala email..Mfano TBS wanakula pesa za watu kwa malaki na hawawasaidii watu kufanikisha biashara zao bali kazi kubwa ni kuwakwamisha kwa visingizio vidogo vidogo. Ingekuwa ni kama hivyo basi Uturuki isingeendelea kiuchumi na kiteknolojia.sio mimi tu, kuna ndugu zangu kama wawili wamesajili kampuni kwa njia ya mtandao, mwingine ofisini aliniambia alisajili jina la biashara, hela amelipia lakini hawafanyii kazi baada ya malipo, ukikaa muda fulani wanakuletea emial kwamba application yako imekuwa cancelled, na maana yake na hela uliyolipa wamekula. wataalamu tuambieni, kuna shida gani au waseme tu watu tuwe tunafunga safari tunaenda jengo la Ushirika tukafanye manual, tuachane na hizi digital twende analogy. inakwaza kuona hili ni shirika la serikali, wafanyakazi wake ni wa serikali, wanakula mshahara wa kodi zetu halafu wanaleta uzembe (sitaki kuita ujinga nitakuwa nimetukana).
1. Issue ya ombi kufutika ni pale ambapo ombi ambalo halikulipiwa linakaa kwenye mfumo kwa siku saba hapo litafutika.Sio mimi tu, kuna ndugu zangu kama wawili wamesajili kampuni kwa njia ya mtandao, mwingine ofisini aliniambia alisajili jina la biashara, hela amelipia lakini hawafanyii kazi baada ya malipo, ukikaa muda fulani wanakuletea email kwamba application yako imekuwa cancelled, na maana yake na hela uliyolipa wamekula.
Wataalamu tuambieni, kuna shida gani au waseme tu watu tuwe tunafunga safari tunaenda jengo la Ushirika tukafanye manual, tuachane na hizi digital twende analogy.
Inakwaza kuona hili ni Shirika la Serikali, wafanyakazi wake ni wa Serikali, wanakula mshahara wa kodi zetu halafu wanaleta uzembe (sitaki kuita ujinga nitakuwa nimetukana).