BRELA
Govt Institution
- Dec 14, 2023
- 119
- 89
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wananchi wa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Ngarenaro, Jijini Arusha, ili kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala huo.
Wito huo umetolewa leo tarehe 15 Septemba 2026 wakati wa Maonesho ya Viwanda Business Clinic yaliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo yanayoendelea katika viwanja hivyo.
Awali, akizungumza katika banda la BRELA, Afisa Leseni wa Wakala huo, Bw. Rajabu Chambega, amesema BRELA imeshiriki katika maonesho hayo mahsusi kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.
“Tumefika hapa Arusha kushiriki katika kliniki hii iliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa lengo la kuwafikia wakazi wa Arusha na maeneo jirani ili waweze kupata huduma zetu kwa urahisi zikiwemo usajili wa majina ya biashara, usajili wa makampuni na utoaji wa leseni,” alisema Bw. Chambega.
Aidha, Bw. Chambega aliwasisitiza wamiliki wa makampuni hususan yanayojihusisha na masuala ya utalii, hoteli na viwanda kuhakikisha wanafuata sheria kwa kusajili na kuhuisha biashara zao kwa wakati.
Katika hatua nyingine, Bw. Chambega, aliwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo kupata elimu kuhusu masuala ya Miliki Ubunifu, Alama za Biashara pamoja na Hataza ili kupata fursa mbalimbali za kibiashara na mikopo.
Maonesho ya Viwanda Business Clinic yanahusisha Taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara zikitoa huduma kwa wananchi wa Kanda ya Kaskazini kwa pamoja.