BRELA
Govt Institution
- Dec 14, 2023
- 119
- 89
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) unapenda kuutaarifu umma kuwa Msajili wa Kampuni ametoa Notisi ya Mwisho ya Nia ya Kufuta Kampuni katika Daftari la Msajili, kwa mujibu wa kifungu cha 403(3) cha Sheria ya Kampuni, Sura ya 212.
Hatua hii imekuja baada ya Msajili kutoa Notisi mbili za awali kwa kampuni husika, ambapo Notisi ya kwanza ilitolewa tarehe 2 Juni 2022 na Notisi ya pili tarehe 13 Julai 2022. Kupitia Notisi hizo, kampuni zilizoorodheshwa zilitakiwa kuthibitisha iwapo zinaendelea kufanya biashara.
Kwa mujibu wa Notisi ya Mwisho iliyotolewa kwenye Gazeti la Serikali Toleo Na 38 la tarehe 18 Septemba, 2026, kampuni zote zilizoorodheshwa kwenye gazeti hilo zimepewa muda wa siku tisini (90) kuanzia tarehe ya tangazo hilo kuwasilisha pingamizi kwa Msajili wa Kampuni dhidi ya nia ya kufutwa kwake.
BRELA inawataka Wakurugenzi, Wanahisa na Makatibu wa kampuni zilizoorodheshwa kuchukua hatua stahiki ndani ya muda uliotolewa, kwa kuwa endapo hakutokei pingamizi lolote baada ya muda wa siku tisini (90) kumalizika, Msajili ataendelea na hatua za kuzifuta kampuni hizo kutoka katika Daftari la Msajili.
Orodha ya kampuni zinazokusudiwa kufutwa inaweza kusomwa kwenye Gazeti la Serikali Toleo Na. 38 la tarehe 18 Septemba, 2026 linapatikana kwenye tovuti ya BRELA yenye kiungo cha mtandao www.brela.go.tz

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma